ZAIDI YA MITI MILIONI MOJA YAPANDWA SENGEREMA,CHANGAMOTO YA TABIA NCHI YATAJWA-HALMASHAURI
Changamoto ya hali ya ukame wa mvua imechangia kupunguza kasi ya upandaji wa miti wilayani Sengerema licha hadi sasa kuwa na zaidi ya miti milioni moja.
Afisa mazingira wa Halmashauri ya Sengerema Tandi Laizer amebainisha kutokana na changamoto hiyo sasa hawana budi kugeukia kilimo cha umwagiliaji ili kuendelea na kampeni ya kuifanya wilaya hiyo kuwa ya kijani.
Amebainisha uwepo wa miti mingi kuna faida nyingi ikiwemo kupunguza hewa ya ukaa angani hivyo watahakikisha wanazidi kuwaelimisha wananchi kuhusu faida ya upandaji miti na hasa Ile inayovumilia ukame.
"Ofisi yangu inawaelimisha wananchi aina ya miti inayofaa kupandwa kwa nyakati kama hizi,na hii ni baada ya kubaini wengi wameingia hasara kutokana na bila kujua mti upi unavumilia ukame na kujikuta inakauka,"Afisa mazingira
Sisi tuna jumla ya miti 1862 tuliyoanza kupanda mwaka jana ikiwemo ya mbao na matunda,lengo letu ni kuwa na mazingira mazuri yatakayo kuwa na tija kwetu,"Mwl Emmanuela Mhekela
Akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuhamasisha umuhimu wa kupanda miti,Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amewataka vijana kujikita katika zoezi hilo ambalo pia ni ajira kwao.
"Nimepitia pita kwa baadhi ya maeneo wilayani humu nimeona mlivyo hamasika lakini bado ongezeni kasi na kuwaelimisha wenzenu bila kujali rika",Balandya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.