Zoezi la uokoaji wa miili iliyozama katika meli ya Mv. Nyerere katika kisiwa cha Ukara linaendelea ambapo mpaka asubuhi ya leo ambapo Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe Waziri wa Uchukuzi Ujenzi na Mawasiliano (MB) anawasili eneo la tukio kuna watu takribani 75 walikuwa wamekwisha okolewa wakiwa wamekufa.
Zoezi la uokoaji linaendelea kufanyika kwa kusaidiana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mwanza na Mkoa wa Mara, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, wapigambizi mbali mbali toka mkoa wa mwanza, kwa kushirikiana na Kamanda Wa Polisi Tanzania IGP Simon Sirro.
"Taratibu za kimila na za kidini zitafuatwa katika kuwasitiri waliofariki kwani msiba huu ni wa kitaifa, hivyo nawaomba wananchi waendelee kuwa wavumilivu na kuanza kuja kuwatambua ndugu zao. Na viongozi mbali mbali wanaendelea kuwasili na kuongeza nguvu katika kusaidia uokoaji Waziri mwenye dhaman ya kamati ya Maafa Mhe. Jenista Muhagama. Maiti nyingi zimejulikana na baada ya muda mfupi miili itaanza kutambuliwa na ndugu zao," alisema Kamwelwe.
Meneja wa TAMESA Mkoa wa Mwanza Eng. Hassan Kalonda ameeleza kuwa Meli hiyo inauwezo wa kubeba uzito wa Tani 25 na ameeleza kuwa wafanyakazi wa kivuko waliokuwepo melini walikua nane (8), na watatu wameokolewa wakiwa wazima na watano wanahofiwa kufariki. Watano hao wanaotajwa kufariki ni Abel Mahatane Nahodha, Agustino Cherehani Fundi, Emmanuel Shinga Karani, Blastus Bundala Mkuu wa Feri na Mathias Thomas Mlinzi.
IGP Simoni Sirro amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu katika shughuli zinazoendelea za uokoaji na amewataka kutojaribu kufanya matukio yakihalifu kwani jeshi la polisi limejipanda na linahakikisha ulinzi unaimarika muda wote.
Miili yote iliyookolewa imehifadhiwa katika kituo cha afya Bwisya kisiwa cha Ukara. Na zoezi la uokoaji linaendelea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.