Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amewataka waajiri na waajiriwa kuhakikisha wanadumisha ushirikiano mwema baina yao pamoja na serikali ili kuhakikisha wanafikia maendeleo endelevu nchini.
Mongella amesema hayo wakati wa sherehe za kusherekea siku ya wafnyakazi Duniani Mei Mosi ambapo kimkoa ilifanyika katika viwanja vya CCM Kirumba kwenye wilaya ya Ilemela,
“Ni ukweli kwamba mkiwa na mshikamano na ushirikiano baina ya waajiri na watumishi itasaidia kutatua kero za wafanyakazi” alisema Mongela.
Mongela alikemea pia tabia ya wajiri kutoa hundi hewa kwa wafanyakazi hodari pamoja na tabia ya waaajiri kukopwa zawadi za Mei mosi akisema mchezo huo uachwe na katu usijurudie tena.
‘’Nakemea sana tabia hii ya kukopa zawadi za washindi wa wafanyakazi bora jambo sio zuri kabisa,mfano mzuri ni ofisi yangu wale wafanya kazi bora wa mwaka jana hawakupewa zawadi zao wamekuja kupewa zawadi za mwaka jana leo asubuhi (Jumatatu)’’ alisema Mongela.
Mkuu wa mkoa aliagiza zawadi za wafanyakazi bora wa wilaya ya Sengerema na Misungwi wapewe zawadi zao za mwaka jana. Pia alipongeza kauli mbiu ya Mei mosi mwaka huu inayosema ‘’Uchumi wa Viwanda,Ulenge Kulinda haki na maslahi na heshima ya mfanyakazi’’.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alisema kauli mbiu hii ni muafaka kabisa katika kutengeneza Tanzania ya viwanda ili kuendana na kasi ya Mheshimiwa rais John Magufuli.
Mongela aliziagiza Halmashauri na wilaya zote mkoani hapa zihakikishe zinaunda mabaraza ya wafanyakazi sehemu ya kazi ili kuhakikisha zinatatua kero mbali mbali za wafanyakazi wake “Halmashauri zote zikae vikao hivyo vya mabaraza kabla ya Oktoba 30 mwaka huu”.
Mratibu mkuu wa Mei Mosi mwaka huu mkoani hapa Meshack Sarota ameomba makampuni ya mbali mbali mkoani hapa yaache mambo ya kuchelewesha mishahara kwa wafanyakazi wao.
Sarota alimuomba mkuu wa mkoa mkoa kuhakikisha anatatua kero mbali mbali za wafanyakazi mkoani hapa ili mkoa uweze kupata maendeleo.
Sarota ameipongeza serikali kwa kuwalipa walimu posho zao pale wanapohamishwa kutoka kituo kimoja kwenda nyingine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.