JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MKUU WA MKOA - MWANZA
 


KARIBU MKOA WA MWANZA

Historia ya Mkoa wa Mwanza ilianza wakati ukiwa chini ya tawala za kitemi za wasukuma, wazinza, walongo, wakara na wakerewe kabla ya ukoloni. Wajerumani walipotawala Tanganyika eneo la Mwanza likawa mojawapo ya wilaya katika himaya ya utawala wa Kijerumani. Utawala wa kikoloni wa Mwingereza ulipokabidhiwa uangalizi wa Koloni la Afrika Mashariki baada ya vita kuu ya Dunia, ulianzisha utawala wa majimbo yaani Provinces. Tanganyika ilikuwa na majimbo ya kiutawala manane (8) na mojawapo likiwa ni Lake Province. Maswa, shinyanga, Musoma na Kwimba. Baadaye Lake Province liligawanywa na kuunda majimbo mawili la Lake Province (Sukuma Land) na Western Province). Utawala wa Mwingereza ulimalizika na Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961. Baada ya uhuru Mwanza iliendelea kuwa sehemu ya Jimbo la Lake Province chini ya mtawala wake kwanza wa jimbo (Provincial Commissioner) aliyeitwa Provincial Commissioner Bw. Walden, ambaye alikabidhi madaraka kwa Richard Wambura. Lake Province liliundwa kwa kujumuisha maeneo ya wilaya za Mwanza, Biharamulo, Bukoba, Soma zaidi.

Takwimu za Haraka

  • Ukubwa wa eneo = 25,233 Km za Mraba
  • Idadi ya watu = 3,062,975
  • Idadi ya Halmashauri = 8
  • Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi = 9
  • Shule za sekondari(I-IV) = 253
  • Shule za sekondari(V-VI) = 25
  • Shule za msingi = 914
  • Hospitali = 15
  • Vituo vya afya = 366
  • Zahanati = 307

MITANDAO YA KIJAMII