Mkoa wa Mwanza umefungua milango ya uwekezaji katika mkoa huo na kuainisha fursa zilizopo kwaajili yakuvutia wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika mkoa kufuatia Jukwaa la Biashara liliwakutanisha wadau kwa siku moja jijini hapa.
Akifungua Kongamano hilo liliwakutanisha wadau kutoka kada zote mkoani hapa, mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, ameahidi kushirikiana na wawekezaji wote ambao wataonesha utayari hasa wakati huu nchi inapoelekea katika uchumi wa kati kwakutia msisitizo katika suala zima la viwanda.
Mongella amesema tayari Mkoa huo umetenga Hekari 11,129.3 kutoka wilaya Nyamagana hekari 1340, Ilemela hekari 189.3 na hekari 650 zinazoendelea kufanyiwa kazi wialayani humo , Misungwi hekari 6000, Magu hekari 1250 na Kwimba hekari 1250, na hekari 500 ambazo bado zipo kwenye mchakato.
Amesema mapango wa mkoa huo nikuona kila Halmashauri kuwa na Viwanda Viwili, ambavyo vitasindika bidhaa zinazotokana na malighafi inayopatikana katika maeneo husika ili kukuza mnyororo wa thamani (value chain) na kuunganisha shughuli za kila siku za Wananchi na Viwanda ili kuongeza tija kwa wananchi.
Mkuu huyo wa mkoa amesema mkoa pia umepanga kuendeleza Eneo la Nyamhongolo kama eneo maalumu la Viwanda. Ambapo EPZA wameendelea mchango mkubwa kwa kuanza kuandaa mpango wa matumizi bora wa eneo hilo la uwekezaji (SEZ) ambao unalenga miaka mingi ijayo.
Akitoa salam za Wizara, Mkurugenzi wa Idara ya habari Maelezo na Msemaji mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, amesema siri kubwa kama mkoa huo unataka kufanikiwa lazima waweke mipango inayotekelezeka kuwa na utendaji kazi wa pamoja na kujiandalia masoko ya uhakika.
Kwa Upande wake Mhariri mtendaji wa TSN Dkt. Jimmy Yonazi, amesema wao kama Wachapishaji wa magazeti ya Serikali, wameamua kutoka na kuwafuta wadau huko walipo ili kuhakikisha adhma ya serikali ya awamu ya tano ya seriakali ya viwanda inafikiwa.
Yonazi amesema walianza na mkoa wa Simiyu na sasawameingia katika mkoa wa Mwanza ili hali tayari mkoa wa Tanga wamewaalika kwaajili yakwenda kuzitangaza fursa za mkoa huo, hivyo ameombwa wawaunge mkono kwakuwa wao wameamua kuanzisha mwendo.
Jukwaa hilo la Biashara lililokutana kwenye mkoa huo unaochangia pato la taifa kwa asilimia tisa na kushika nafasi ya pili ukitangauliwa na Dar es Salaam, limewakutanisha wadau kutoka nyanja zote za uchumi wakiwapo wafanyabiashara, wakuu wa Taasisi za Serikali, Wakulima, Waendesha bodaboda na Watumishi wa Umma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.