• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mwanza Yaweka mikakati ya kuboresha uzalishaji,mazao ya Kilimo na masoko

Posted on: October 16th, 2020

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Tutuba,amewataka  wakulima  kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA)  ili kupata taarifa sahihi za kiwango cha mvua waweze kuchagua aina ya mazao watakayolima.

Tutuba ametoa  rai hiyo leo wakati akizungumza na wadau wa sekta ya kilimo Mkoa wa Mwanza, kutoka taasisi za Serikali na binafsi  kwenye mkutano ulioandaliwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  uliolenga kujadili changamoto zilizopo katika sekta hiyo ili kuboresha uzalishaji na masoko ya mazao ya biashara na chakula.

 Alisema ukosefu wa taarifa sahihi za  hali ya hewa ni miongoni mwa changamoto zinazosababisha wakulima kuvuna mazao kidogo kwa sababu  wanalima mazao bila kujua kiwango cha mvua kitakachokuwepo mwaka husika wa kilimo.

” Serikali  inaweka mazingira wezeshi kwa wakulima lengo ni kila mkulima afaidike na shughuli hiyo, lakini baadhi yao wanakosa taarifa sahihi za hali ya hewa  kuna mazao hayahitaji mvua nyingi na mengine yanahitaji mvua chache.

“Ili mkulima aweze kuamua zao lipi alime kulingana na kiwango cha mvua kwa mwaka husika ni wajibu wetu sisi wadau wa sekta ya kilimo wote wa taasisi za Serikali na binafasi kuwafikishia taarifa hizo kutoka TMA,”alisema.

Alisema Mkoa wa Mwanza unazo fursa nyingi za kilimo  ikiwemo mvua za kutosha na ardhi yenye rutuba pia ni kitovu cha  masoko hivyo wakizitumia vizuri wakulima wengi watanufaika kwa kufanya kilimo biashara.

“Lazima tuwe wabunifu tuangalie ni changamoto gani zinazosababisha tija iwe ya chini,  jukumu letu sisi wadau wa kilimo  tuzibainishe,  tuwaelekeza na kuwashawishi wakulima wetu wazingatie kanuni bora kilimo .

Aliwashauri wadau hao kuwafundisha wakulima kutunza takwimu za gharama walizozitumia katika kilimo ili wahakikishe wanalima mazao ambayo yatawaingizie kipato na si kuwapa hasara.

Miongoni wa mazao yatakayopewa kipaumbele katika Mkoa wa Mwanza  ni pamoja na mahindi, pamba, mtama, alizeti, mpunga, muhogo, dengu mboga na matunda.

Matangazo

  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MKOA WA MWANZA MWAKA 2021 December 18, 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza 2018 Shule za Sekondari za Serikali Mkoa wa Mwanza December 13, 2017
  • Ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji katika shule za Msingi na Sekondari Mkoa wa Mwanza 2018 January 10, 2018
  • Ufunguzi wa Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA Kitaifa Mkoa wa Mwanza. June 07, 2018
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AGA KHAN Yatoa Vifaa vya Bilioni 1.5 Kuepusha vifo vya mama na mtoto Mwanza

    December 22, 2020
  • Kikao cha bodi ya Barbara chapanga mikakati ya mafanikio Mwanza

    December 21, 2020
  • Mwanza Kwanza Toleo la pili kwa habari mbalimbali Mkoa wa Mwanza

    December 12, 2020
  • Elimu ya maadili yatolewa Mwanza kwa Viongozi

    December 10, 2020
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella akifungua Baraza la biashara katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkikutano uliopo katika ofisi ya Mkoa uliojumuisha wajumbe mbalimbali wa Baraza hilo wa Mkoa wa Mwanza.
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Regional Drive Mkabala na Ofisi za TRA

    S.L.P: S.L.P. 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.