Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameipongeza sekta ya elimu mkoani humo kwa kupandisha ufaulu wa wanafunzi katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita 2025 kwa asilimia 99.92 kwa daraja la 1 hadi 4 kutoka asilimia 99.7 mwaka 2024.
Mhe. Mtanda ametoa pongezi hizo leo Julai 09, 2025 wakati akiongea na wanahabari na wataalamu wa idara ya elimu katika kikao cha tathmini ya matokeo ya mtihani wa kidato cha sita ndani ya halmashauri nane za mkoa huo.
Amebainisha kuwa Sengerema Sekondari imekua kinara kwa kufaulisha kwani wanafunzi wote zaidi ya 600 wamepata daraja la 1-3 na kutokua na daraja la 4 wala sifuri huku Nsumba sekondari wakishika nafasi ya 2 na Bwiru wasichana wakishika nafasi ya 3.
“Natoa pongezi kwa wataalamu wa Idara ya Elimu, Wazazi na wanafunzi wenyewe kwa juhudi zao binafsi kwani tukichukulia wanafunzi waliofaulu daraja la 1 ni 3013 sawa na 53% kwa mwaka huu wakati mwaka 2024 walifaulu kwa 50% pekee.” Amesema Mhe. Mtanda.
Aidha, amefafanua kuwa wanafunzi 3 kutoka Sengerema wamepata Daraja la 1 kwa alama 3 za ufaulu huku Nsumba sekondari akipatikana mmoja na kwamba Mkoa utawapongeza rasmi wanafunzi hao pamoja na wazazi/walezi na walimu.
Katika vituo 99 vyenye watahiniwa 5767, jumla ya watahiniwa 5690 mwezi mei 2025 walifanya mtihani huo ambayo ni sawa 98% huku 2% wakishindwa kufanya kutokana na sababu mbalimbali na kwamba Julai 07, 2025 NECTA ilitangaza matokeo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.