Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, amekemea na kuwalaani baadhi ya Maafisa uvuvi wasio waaminifu na wanaoshirikiana na wavuvi haramu mkoani hapa.
Akizungumza kwenye eneo la Mwaloni Kirumba kufuatia tukio la kukamatwa kwa samaki kilogram 3482 wenye thamani ya Mil.20,892,000/= wasiokidhi vigezo, Mongella amesema, vita hivyo haviwezi kufanikiwa ikiwa Maafisa uvuvi wataamua kushirikiana na Wavuvi hao haramu.
"Kama Maafisa wa Serikali, wakiwa ndio vinara wakuwasaidia wavuvi haramu ni bora tukafanye kazi zingine, maana kama ni kazi zakufanya zipo nyingi, alisema Mongella na kuongeza kuwa."
Haiwezekani TAKUKURU, wakamate Mhalifu, waondoke na kibali chakusafirishia mzigo husika, halafu wewe Ofisa wa Uvuvi uruhusu samaki waindoke bila kibali na isitoshe mhusika hana Leseni, kwa nn tusiseme upo kwenye payroll ya wahalifu?". Alihoji mkuu wa Mkoa.
Mongella aliyasema hayo kufuatia, Maelezo yakubabaisha yaliyotolewa na Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya ILEMELA, Bw. Ivon Maha, kumwambia Mkuu wa mkoa kwamba kufuatia kukamatwa kwa Samaki hao na Taasisi ya kupambana na Rushwa, wao kama wataalam wa masuala ya samaki waliwachambua na kisha kubaini kilo 2,316 wenye thamani ya Shilingi 13,896,000 walikuwa wanakidhi viwango, hivyo kwakushirikiana na Maafisa wa TAKUKURU wakaruhusu samaki hao wachukuliwe na mhusika. Hata hivyo kauli iliyo kanushwa vikali na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza bw. Ernest Makale mbele ya Mkuu wa mkoa.
"Mhe. Mkuu wa Mkoa, sio kweli kwamba TAKUKURU, tullishiriki kuwaachia samaki hao walio chambuliwa, kwani sisi mara baada yakuwatia mbaroni wahusika, tulichofanya nikuwaita waatalaam wavuvi na kuwakabidhi samaki lakini tukaenda mbali zaidi, kibali kibali husika kilichokuwa kinatumika kuwasafirishia samaki hao tukaondoka nacho na tunacho kibali hicho" alisema Makale.
Hali hiyo ilizua maswali kwa Mkuu wa Mkoa na kuanza kumhoji afisa uvuvi huyo, ilikuwaje aruhusu mzigo uachiwe ili hali kibali kilikuwa chini ya TAKUKURU? na Isitoshe Mtuhumiwa Mageta Bigambo ambaye ni Mtuhumiwa wa biashara hiyo inasadikika hana Leseni ya Biashara na kibali alichokuwa nacho kilikuwa chini ya TAKUKURU. Alihoji mkuu wa Mkoa.
Mara baada ya Maelezo Mkuu wa Mkoa aliliagiza jeshi la Polisi kumchukua Afisa Uvuvi wa Manispaa hiyo kwaajili ya mahojiano zaidi ili ukweli uweze kufahamika.
Kwa Mujibu wa Sheria ya Uvuvi na 22 ya Mwaka 2003 na kanuni zake za Mwaka 2009 ni makosa kuvua samaki sangara Wadogo waliochini ya Sentimita 50 ambao wanatajwa kama samaki wadilogo, na pia marufuku inakataza kuvua samaki walio zaidi Sentimita 85, ambao huuchwa kwaajili ya Mazalia samaki.
Mkoa wa Mwanza upo katika Mapambano ya vita dhidi ya Uvuvi haramu ambapo tayari Wavuvi haramu, Nyavu za makila na Zana zingine za uvuvi zimesha kamatwa kwenye maeneo Buchosa, Ilemela na Sengerema na kuteketezwa kwa Nyakati tofauti.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 33180, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras.mwanza@tamisemi.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.