Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amefungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo na kuwakumbusha wajumbe kuwa baraza la wafanyakazi ni kiunganishi kati ya Menejimenti na wafanyakazi.
"Wajibu wa mabaraza kama chombo cha ushauri na usimamizi ni kuhakikisha kuwa waajiri na watumishi wanatambua wajibu na haki zao,pia wanazingatia maadali ya utumishi wao ili kuleta matokeo ya utendaji yenye tija,staha na upendo,"alisema Mongella.
Awali akitoa ufafanuzi wa umuhimu wa kikao cha baraza la wafanyakazi Mhe.Mongella amesema kipo kisheria kwa lengo la kuishauri Serikali katika ngazi za idara na taasisi kuhusu usimamizi wa kazi na rasilimali watu,utekelezaji wa majukumu,kulinda haki na wajibu wa mwajiri n wafanyakazi,kutoa ushauri kuhusu kujenga hali bora za kazi,maslahi ya wafanyakazi na kusimamia haki na ustawi katika sehemu za kazi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.