CMG KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 1 KUBORESHA MAISHA YA WATOTO VILLAGE OF HOPE MWANZA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 07 Machi, 2025 ametembelea kituo cha malezi ya watoto wenye mahitaji maalumu cha Village of Hope kilichopo Nyegezi Jijini Mwanza kukagua maendeleo ya kituo hicho.
Akizungumza baada ya ukaguzi, Mhe. Mtanda amewapongeza kwa kuanzisha kampeni ya Ndoto za Taifa inayolenga kuboresha miundombinu ya padarasa, mabweni, matundu ya vyoo na maji kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Clouds Media Group (CMG)
Mhe. Mtanda amesema kampeni hiyo inaonesha kujali watoto wenye mahitaji maalum na akatumia wasaa huo kuwapongeza CMG kwa kuitangaza ili kuchagiza wadau mbalimbali kushiriki kuchangia ndoto za watoto hususani afya na lishe.
Akisoma risala ya Village of hope Bi. Grace Obandu amewashukuru CMG kwa kufufua matumaini mapya na kudumisha kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalumu kwa kuamua kushirikiana nao katika kuboresha miundombinu ambapo zaidi ya watoto 1300 wanahudumiwa kwa vituo viwili vya Mwanza vya Nyegezi na Bulale - Buhongwa.
"Kituo chetu kilianza Januari 2012 chini ya msaada wa wahisani kutoka makanisa ya Pentekoste ya nchini Canada kwa lengo la kusaidia watoto kutimiza ndoto za maisha kupitia malezi ya kiroho na kiakili." Bi. Grace.
Mwakilishi wa CMG Kanda ya ziwa Malkia Sarah Onesmo amesema wao kama kitovu cha maarifa wana furaha kushirikiana na Serikali katika kuchangia maendeleo ya watoto chini ya mwamvuli wa Moyo wa Mawingu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.