Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana Taasisi ya Benjamini Mkapa na Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kupitia mradi wa Mfuko wa dunia wa kupambana na magonjwa ya Kifua kikuu,Malaria, na HIV/AIDS(GFATM)na mradi wa Mkapa Fellows Program awamu ya tatu,imeendesha kikao kazi cha kukamilisha mchakato wa ajira na kuwapangia vituo vya kazi wataalamu mbalimbali wa kada za afya ambao wanatakiwa kuripoti katika vya kazi kuanzia Septemba 25, 2018.
Akiongea katika kikao hicho cha watumishi wa ajira mpya kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bwana David M. Mnkhally Afisa kutoka Taasisi ya Benjamini Mkapa amesema orodha ya majina ya watumishi wote waliopangiwa vituo vya kazi yanapatikana kupitia tovuti ya OR- TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz pia katika tovuti yaTaasisi ya Benjamini Mkapa ambayo ni www.mkapafoundation.or.tz.
Mradi huu wa RSSH unatekelezwa katika Mikoa kumi ya Tanzania bara, Mikoa hiyo inajumuisha Mwanza,Shinyanga,Mara,Simiyu,Geita,Kagera,Tabora,Katavi,Kigoma na Dodoma.Ambapo jumla ya watumishi 281 wataajiriwa katika Halmashauri mbalimbali katika Mikoa tajwa hapo juu,kwa Mkoa wa Mwanza jumla ni 23, kupitia mradi wa RSSH 19 na MFP III ni 4.
Naye Miyeye Yahya ambaye ni Afisa kutoka Taasisi ya Mkapa ameongeza kuwa ajira hizi ni za mkataba wa mwaka mmoja na zinasimamiwa na Taasisi ya Benjamini Mkapa hivyo basi watumishi wote waliopata fursa hii watapata kipaumbele cha kujiunga na utumishi wa Umma baada ya kukamilika kipindi cha mkataba,kulingana na upatikanaji wa ajira.
Aidha Bwana Deogratias Kayombo ambaye ni Afisa Utumishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na Watoto (Afya) amesema kila mtumishi ahakikishe anazingatia misingi ya uwajibikaji na kukidhi maadili ya utumishi wa Umma katika utoaji wa huduma kwa Jamii.
Hata hivyo, Bi Hawa Waziri ambaye ni Afisa Utumishi Wizara ya Afya amesisitiza utii wa sheria katika Masuala kazi na nidhamu ambapo amewataka watumishi kufanya kazi kwa weredi bila kubagua mtu yeyote katika kutimiza wajibu wao.
"Hakikisheni mnatimiza wajibu wenu na kuukamilisha kwa muda uliopangwa na kwa weredi,haitakiwi kutoa huduma kwa upendeleo fulani ikiwa ni pamoja na ushawishi wa kisiasa au kidini,"alisema Hawa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.