Maadhimisho ya Siku ya Unywaji wa Maziwa Shuleni kufanyika Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani kwenye maadhisho ya siku ya unywaji wa maziwa shuleni yatakayofanyika kwenye viwanja vya furahisha jumatano ya Septemba 27, 2023.
Mhe. Makilagi ametoa wito huo leo tarehe 23 Septemba 2023 wakati wa mkutano wa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla na waandishi wa habari ambapo alizungumza kwa niaba yake kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Aidha, Makilagi amesema unywaji wa maziwa shuleni unachangia kuwapa afya njema watoto, kuboresha ukuaji wa mtoto, kupata matokea mazuri kwenye taaluma, kuanza mapema tabia ya umuhimu wa matumizi bora ya lishe, kuhudhuria masomo bila kukatisha na kuondoa utoro.
"Maziwa yanasidia kumfanya mtoto kuwa na afya bora na hali hii inachangia sana hamasa ya kujifunza na kuwafanya watoto kupenda shule tofauti kabisa na watoto wasiopata maziwa shuleni na watoto wakijengwa hivyo inasaidia kupanua ufaulu." Amesema Mhe. Mkuu wa Wilaya.
Vilevile, amefafanua kuwa kilele cha maadhimisho hayo kitatanguliwa na shughuli mbalimbali kama ugawaji wa maziwa kwenye shule kumi za watoto wenye mahitaji maalum zaidi ya 450 siku ya tarehe 25, Septemba 2023 na siku ya jumanne kutakua na kongamano la wadau kuhusiana na maadhimisho hayo katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.
"Hali ya unywaji wa maziwa kwa sasa nchini bado iko chini kwani kwa mwaka inatakiwa mtu anywe lita 200 lakini mtanzania kwa sasa anakunywa lita 62 tu na lengo la maadhimisho haya ni kutoa elimu ya umuhimu na kuhamasisha watu kunywa maziwa." Amesema Deogratias Buzuka, Afisa uzalishaji Maziwa Bodi ya Maziwa Tanzania.
Katika kuchagiza matumizi bora ya maziwa kwa ukuaji na kujenga siha njema kwa jamii, maadhimisho ya siku ya unywaji wa maziwa nchini mwaka 2023 yanaenda na Kaulimbiu isemayo 'Mpe Mtoto Maziwa kwa maendeleo bora shueni'.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.