Kufuatia ajali ya moto iliyotokea Novemba 20, 2025 na kuunguza mabweni mawili ya Shule ya Sekondari Sumve, juhudi za pamoja zimeendelea kuleta matumaini mapya kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Akizungumza leo Januari 16, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amempongeza Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw. Elikana Balandya kwa jitihada zake za kutafuta wadau na wahisani waliowezesha upatikanaji wa msaada kwa shule hiyo.

Kupitia mchango huo, magodoro 219 yenye thamani ya shilingi milioni 10. 5 yamekabidhiwa kwa uongozi wa shule ambapo kila godoro lina thamani ya shilingi 48,000.

Mhe. Mtanda amesema msaada huo utasaidia kurejesha mazingira bora ya malazi kwa wanafunzi walioathirika na tukio hilo la moto.

Aidha, amewashukuru wadau mbalimbali waliotoa mchango wao pamoja na wananchi wa eneo la Sumve kwa ushiriki wao wa haraka katika kuzima moto hatua aliyosema imepunguza madhara zaidi.

Amesisitiza kuwa mshikamano huo ni mfano wa kuigwa katika kukabiliana na majanga na kuunga mkono sekta ya elimu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.