Makatibu Tawala Wasaidizi, Maafisa Kilimo kanda ya Ziwa wapata mafubzo upatikanaji Pembejeo
Makatibu Tawala wasaidizi upande wa uzalishaji na uchumi kutoka mikoa ya Mwanza,Simiyu,Shinyanga na Geita pamoja na Maafisa Kilimo wametakiwa kuja na matokeo chanya baada ya kupatiwa mafunzo ya mradi wa upatikanaji wa Pembejeo za kilimo nchini maarufu kama TAISP.
Akifungua mafunzo hayo leo Oktoba 30,2023 kwenye ukumbi wa mikutano wa TFDA Buzuruga Mkoani Mwanza,mwakilishi wa Mkurugenzi Sekta za Uchumi na Uzalishaji kutoka Tamisemi,Bi. Hofu Mwakaje amesema mradi huo uliolenga zao la mpunga kwa mikoa hiyo una nia ya kuleta tija kwa wakulima wanawake na vijana.
Amebainisha baada ya kufanyiwa kazi changamoto zilizochangia kuzorota kwa zao la mpunga likiwemo ukosefu wa mbegu bora na mbolea,sasa Maafisa hao wana wajibu wa kusimamia vyema kilimo hicho.
"Mradi sasa umewatumia vyema wataalamu kutoka Taasisi za kilimo kwa kuzifanyia utafiti mbegu bora na mbolea za kisasa na kuwawekea mazingira rafiki Maafisa ugani wote ili malengo ya uzalishaji wenye tija upatikane",Bi.Hofu
Awali akiwakaribisha Maafisa hao mwenyeji wa kikao hicho ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji,Emil Kasagara amempongeza Rais Samia kwa kufanya uwekezaji mkubwa kwenye Sekta ya Kilimo,hivyo wahusika wana wajibu wa kuwajibika ipasavyo.
"Mradi huu wa miaka 5 umewalenga jumla ya wakulima 1,200,000 uonafadhiliwa na JICA kwa zao la mpunga kwa mikoa 4 na ADB mikoa 10 kwa mazao ya ngano na alizeti,"Lisa Chawe,mratibu wa mradi.
Mshauri wa mradi wa upatikanaji wa Pembejeo za kilimo TAISP, Deo Mavika amesema sababu ya mradi huo hapa nchini ni kutokana na vita vya Urusi na Ukraine Mataifa ambayo ni wazalishaji wakubwa wa ngano ulimwenguni,ugonjwa wa Uviko na Uzalishaji hafifu wa mazao hayo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.