• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mapambano dhidi ya ukatili kwa watoto Yaendelea

Posted on: July 17th, 2019


Mapambano dhidi ya ukatili na  mimba za watoto shuleni katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani  Mwanza yameoneka kutokuwa mafanikio chanya  baada ya takwimu kuonyesha  kuongezeka kila mwaka.

Hayo yamebainishwa  jijini Mwanza katika  semina  iliyoandaliwa na Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto (KIVULINI) kwa taasisi  mbalimbali  zikiwamo ya  mwendesha mashitaka mkoa,  mahakama, askari wa dawati la jinsia, wapelelezi,  ustawi wa jamii na mashirika  binafsi yanayojihusisha na utetezi  wa haki za binadamu, uzuiaji wa vitendo vya ukatili.

Akiwasilisha taarifa za  matukio ya ukatili na mimba za  watoto , Mkuu wa dawati la Jinsia kutoka Polisi Mkoa wa Mwanza, Berth Shija alisema mwaka 2017 walipokea kesi 1,287 na zilizofikishwa kitengo cha upelelezi ni 1,200 ambapo  9 zilikosa ushahidi.

Alisema   kati ya kesi   1,200 zilizokuwa zikifanyiwa upelelezi, kesi  59 ndizo zilifikishwa  mahakamani na kati ya hizo 19 ndiyo zilifanikiwa.

“Mwaka 2018 taarifa zilizopokelewa ni  1,682, zilizofika kitengo cha upelelezi ni 1,263, zilizokosa ushahidi 142 na zilizofikishwa mahakamani 278 lakini kati ya hizo zilizofanikiwa kwa kupata ushindi mahakamani ni 36 pekee.

“Mwaka huu 2018 kuanzia  Januari  mpaka sasa tumepokea kesi 1,012, zilizofikishwa kwenye upelelezi 827, zilizokosa ushahidi   ni sita ambapo zilizofikishwa mahakani 179  na hatujaweza kujumlisha kwani hatujapokea taarifa kutoka wilaya zote za mkoa wetu wa Mwanza,”alisema Shija.

Kwa upande wa Mkuu wa Dawati la Jinsia kituo cha Polisi Kirumba, Rico Ndaro alisema matukio ya mimba kwa wananfunzi kuanzia mwaka 2016  yalikuwa 17 lakini 2017 yalikuwa 31, 2018 yalikuwa 41 ambapo  kwa mwaka huu yamepokelewa 28 kati ya Januari hadi Juni.

“Kwa miaka mitatu iliyopita jumla ya kesi 96 ziliripotiwa kituo cha polisa kirumba na kesi 44 zilifikishwa mahakamani  ambapo kati ya hizo 21 zilishinda mahakamani ambapo katika kesi hizo watuhumiwa 18 walifungwa kila mmoja miaka 30 jela.

“ Watuhumiwa  wengine  wawili  walifungwa  kifungo cha maisha jela na mmoja alifungwa miaka 35 jela ambapo jumla ya kesi 23 ziliondolewa mahakamani kwa kukosa ushahidi.

“Kati ya kesi  96 zilizopokelewa Kirumba,  kesi 52 ziliishia polisi kwa kukosa ushahidi lakini  jumla ya kesi 36 zilitokea  hasa katika maeneo ya  Igombe na Kayenze Wilaya ya Ilemela,”alisema.

Wakichangia mada  ya mkakati wa kukomesha vitendo hivyo na kufanikisha kesi  hizo, wadau mbalimbali walionekana kulalamikia kitengo cha upelelezi na madaktari kushindwa kujaza  vizuri fomu namba 3 ya polisi (PF3)  na kutofika mahakamani ili kutoa ushahidi.

Mrema Juma kutoka  kutoka ofisi ya  mpelelezi Wilaya ya Ilemela alisema  ni kweli baadhi ya kesi zinaishia hapo au kukaa muda mrefu kutokana na kukosa ushirikiano na watu ambao ni wahusika hivyo aliwataka wadau wote wanaohusika na mlolongo wote wa kufanikisha kesi hizo kushirikiana.

Baadhi ya madaktari waliochangia walisema kuwa si wote wanaokataa kwenda mahakamani kutoa ushauri isipokuwa wachache wanaokwenda hupata usumbufu mkubwa kutoka kwa mahakimu  kwa kukaa muda mrefu na hata kesi kuahirishwa bila kuitwa.

Pamoja na michango yao, waliiomba mahakama kuanza na kesi za mimba na ukatili kwanza ili kuwapa nafasi ya kuwahi kurudi katika majukumu yao ya kuwahudumia wananchi katika maeneo yao ya kazi badala ya kusota mahakamani.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.