Leo Agosti 29, 2025 Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Jitihada vilivyojengwa kwa fedha zilizotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Tshs. Milioni 50.
Bwana Ussi amesema amefurahi kuona Halmashauri imeweka mkakati wa kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuinua ari ya ujifunzaji na ufundishaji na amesema kuwa matarajio ya Serikali ni kuona kiwango cha ufaulu kitaendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka.
Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Johari Samizi amesema ujenzi wa madarasa hayo ulianzishwa ili kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuhakikisha wanafunzi wote watakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2026 wanapata nafasi.
Vilevile, Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa barabara ya Majengo (Km 0.5) kwa kiwango cha lami nyepesi unaogharamiwa kwa fedha za tozo ya mafuta na unatekelezwa na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini - TARURA chini yaMkandarasi M/S Mumangi Construction Company Limited, kwa gharama ya Tshs. 411,013,450.00.
Matengenezo ya barabara hiyo yatapunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mara kwa mara wa barabara hivyo kupunguza gharama za matengenezo ya mara kwa mara, kadhalika matengenezo hayo yamebadilisha taswira ya mji wa Misungwi, yameboresha hadhi ya makazi pamoja na kuboresha huduma ya usafiri na usafirishaji na kupekelekea kuvutia mazingira ya Uwekezaji.
Kadhalika, umezindua huduma za Afya na vifa tiba vya kisasa katika Zahanati ya Nyamikoma ambavyo vitasaidia wananchi kupata tiba sahihi na ya kitaalamu na kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka 5 vilivyokuwa vikisababishwa na kutembea umbali mrefu kwenda Hospitali ya Wilaya na Zahanati za Vijiji ya jirani kutafuta huduma za Afya.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.