Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg. Ismail Ali Ussi ameupongeza Uongozi wa Wilaya ya Misungwi kwa kutekeleza Mkakati wa Taifa wa matumizi ya Nishati safi ya kupikia ya mwaka 2024 - 2034 kwa kuhamasisha na kutoa Elimu kwa jamii juu ya matumizi sahihi.
Ndugu Ussi Ametoa pongezi hizo leo tarehe 29 Agosti, 2025 katika kijiji cha Iteja wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika katika shule ya sekondari ya Aimee Milembe na kukagua matumizi ya nishati safi ya kupikia ambapo imesimikwa miundombinu ya kisasa inayotumia gesi ya asili.
Ndugu Ussi amesema kwa kuelimisha jamii Wilaya hiyo inatelekeza vema na kwa vitendo kampeni ya nishati safi ya kupikia Kitaifa na Kimataifa inayolenga kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kupunguza athari za kimazingira.
Aidha, amebainisha kuwa masuala ya nishati safi ya kupikia pamoja na afua zingine za kukabiliana na athari za kimazingira ni utekeleza wa agenda ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkakati wa kuhakikisha 80%ya watanzania wanatumia nishati safi ifikapo 2034.
Naye, Mkuu wa wilaya ya Misungwi Mhe. Johari Samizi amesema wilaya hiyo ina vikundi 4 vya wanawake vinavyozalisha wastani wa majiko banifu 200 kwa Mwezi, kaya 11,567 zinazotumia gesi (LPG) kwa ajili ya kupikia, Migahawa 3 na Taasisi 3 za Elimu.
Mhe. Samizi ameongeza kuwa chini ya ushirikiano na mdau wa maendeleo Africa School House wameweza kuokoa gharama ya kupikia kutoka shilingi 500,000 ziizokuwa zikitumuika awali kununua kuni hadi shilingi 300,000 zanazotumika sasa kununua Gesi kwa mwezi.
Kabla ya kukagua matumizi ya nishati safi katika shule hiyo mwenge wa uhuru umezindua klabu ya kupambana na rushwa ambapo wanafunzi wamejipanga kutoa elimu kwa wenzao na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanapambana na udhalimu wa matendo ya rushwa ambayo yanaathiri uzalendo na kupelekea ubadhirifu wa mali za umma.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.