• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Mfumo wa maisha kuwa chanzo shinikizo la damu - Dkt.Rudovick

Posted on: May 15th, 2021

Zaidi ya asilimia   90   ya watu wenye umri wa miaka kati ya 30  hadi 50 wanaopatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu chanzo chake bado hakijulikani mpaka sasa.

Aidha,  watu  wenye umri wa  chini ya miaka 30  na zaidi ya  miaka 55 chanzo cha wao kupatwa na ugonjwa huo kinajulikana na kikiondolewa tatizo linakwisha.

Takwimu hizo zilitolewa  na daktari bingwa  wa magonjwa ya figo na shinikizo la damu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Ladislaus Rudovick.

Alisema ugonjwa wa shinikizo la damu umegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni msingi (primary) na sekondari (secondary).

 Katika siku ya Shinikizo la Damu Duniani, hospitali ya Bugando ilitoa   huduma za upimaji afya bure kwa magonjwa yasiyoambukizwa.

Dk.Rudovick alisema  kila tatizo la kiafya linatibika ikiwa mgonjwa akiwahi kupata matibabu .

Alivitaja baadhi ya visababishi vya ugonjwa huo ni pamoja na  mishipa ya kwenye figo kuwa miembamba,  uvimbe tumboni na matatizo ya tezi yanayosababisha homoni mwilini kuongezeka pamoja na mfumo wa maisha.

Kwa mujibu wa Dkt.  Rudovick, mfumo wa maisha unaweza kuwa chanzo kikubwa hasa kwa watu wenye kipato kizuri kinachowafanya kula  ulaji usiopangiliwa pamoja na kukosa muda wa kufanya aina yoyote ya mazoezi, japo ya kutembea.

“Utakuta mtu anatoka ndani kwake na kuingia kwenye gari hadi ofisini. muda wa kazi ukiisha anaingia tena kwenye gari,  anapita sehemu za burudani, anaagiza nyama, tena ile nyekundu na kileo, hasa bia, kisha anarudi nyumbani anaoga na kulala na kesho yake hivyo hivyo,”  alisema

Alisema suluhisho la kwanza kwa mtu mwenye tatizo la shinikizo la damu ni kufanya mazoezi na kuepuka ulaji usiopangiliwa huku akitoa tahadhali wanaotumia  tiba asilia ambazo hazijafanyiwa utafiti.

Dk. Rudovick,  alisema tiba asili zisizofanyiwa uchunguzi zinasababisha  madhara mengine yanayoweza kusababisha matatizo ya kiafya ikiwemo kuharibu figo.

Katika maadhimisho hayo pia  uchunguzi wa magonjwa ya ngozi ulifanyika huku,  Dk.   Nelly Mwageni akisema kwamba magonjwa hayo nayo  huendana na umri wa mtu.



Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.