MGANGA MKUU WA MKOA AKABIDHIWA RASMI OFISI AAHIDI USHIRIKIANO NA WELEDI WA KAZI
Aliyekuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoa wa Dodoma Dkt. Thomas Rutachunzibwa amekabidhi rasmi Ofisi kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba aliyehamishiwa mkoani humo akitokea Mkoa wa Kigoma.
Akizungumza leo Julai 8 mara baada ya kukabidhiwa Ofisi Dkt. Lebba ameonesha kufurahishwa na mapokezi mazuri kutoka kwa wenyeji wake huku akisisitiza ushirikiano na kufanya kazi kwa weledi ili kuzidi kutoa huduma bora katika sekta ya afya.
"Mimi niwaombe tuendelee kushirikiana zaidi na zaidi, ninajua mna ushirikiano lakini tuongeze"Mganga mkuu
Aidha Mganga Mkuu huyo amewataka viongozi na wasimamizi mbalimbali wa Idara ya afya walioshiriki katika makabidhiano ya ofisi kuendelea kufanya kazi kama timu kwani kwa kufanya hivyo inarahisisha kazi.
"Tuongeze kasi ya mafanikio zaidi, tufanye kazi zenye matokeo halisi lakini pia tufuate sheria, taratibu na kanuni". Amesema Dkt. Lebba.
Naye aliyekuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Rutachunzibwa amesema anaamini ameiacha ofisi katika mikono salama kwani anamfahamu vizuri Dkt. Lebba na anamini katika ufanisi wa utendaji kazi wake hivyo ametaka apatiwe ushirikiano wa kutosha.
"Ninaamini tulishirikiana vizuri sana na ninawaombeni mumpatie ushirikiano wa kutosha Dkt. Lebba kama mliokuwa mkinipatia mimi".Dkt. Rutta
Aidha Dkt. Lebba ameitambulisha rasmi kauli mbiu watakayokuwa wakiitumia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku isemayo "Mwanza Safi ya Kijani" kwa kuwataka wasimamizi wote wa afya katika ngazi zote kuhakikisha maeneo wanayoyasimamia wanapata rangi ya kijani tu ambayo inaashiria kufanya vizuri.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.