Mkemia Mkuu wa Serikali afanya Mazungumzo mafupi na RAS Mwanza
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Balandya Elikana leo Machi 4, 2024 amefanya mazungumzo mafupi na Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko ambaye yupo katika ziara ya kutembelea makampuni wanayoshirikiana Katika utendaji wa kazi kanda ya ziwa.
Katika Mazungumzo hayo Balandya amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wanashirikiana nazo kuhakikisha shughuli zote zinazohusisha kemikali zinafuata taratibu zilizowekwa.
"Natambua maeneo ya Kanda ya ziwa kuna shughuli nyingi zinazohusisha kemikali hivyo Katika ziara yangu nitatembelea maeneo yote ya migodi na kwenye mialo", amesema Mkemia Mkuu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.