Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, amesema mbali na kumaliza suala la kushughulikia suala la kiwanda cha Ngozi cha Mwanza Tanneries hivi sasa suala lililopo mbele yake hivi sasa nikushughulikia viwanda vingine vilivyo binafsishwa lakini wahusika wakashindwa kuviendeleza hadi sasa.
Mongella ametoa kauli hiyo Jiji Mwanza mapema wiki hiki hii alipofika katika kiwanda cha Ngozi cha Mwanza Tanneries kwaajili yakutanzua sintofahamu ya nani mmiliki halali wa kiwanda hicho kufuatia sintofahamu iliyokuwa imegubika kwa muda mrefu.
“Nimesha pokea orodha ya viwanda vilivyo binafsishwa kutoka kwa msajili wa hazina, nasema hivii, hatutaishia hapa alisema Mongella na kuongeza “MWATEX, tunakwenda, na nimeambiwa kunakiwanda kingine kipo jirani na MWATEX kinaitwa Pamba Engineering huko tutakwenda” na viwanda vyote ambavyo serikali iliwapa watu kuendesha kwa nia njema lakini wameshindwa lazima hatua stahiki zichukuliwe.
Mongella amesema mbali na kuchukua fungua za kiwanda cha Ngozi cha Mwanza, vilevile mali zote zote za Mwanza Tanneries zitarejeshwa ikiwapo nyumba tatu zilizopo eneo la Bugando.
“Kuna nyumba tatu zipo Bugando zinakaliwa na familia sita, nasema walipo katika nyumba hizo waweke utaratibu wa kukabidhi hizo na tutatafuta mali zingine za Mwanza Tanneriea popote pale zilipo.
Suala la kukirejesha kiwanda hicho cha Ngozi mikononi mwa serikali imechukua siku 29 baada ya mkuu wa mkoa kufanya ziara kiwandani hapo kwa mara ya kwanza tarehe 10, 20, Julai 2017 na kisha akarejea na majibu tarehe 09, August, 2017 akiwa na majibu sahihi kuwa kiwanda hicho hakikuwahi kubinafsishwa.
Katika hatua nyingine, waliokuwa wakijifanya ni wamiliki halali wa kiwanda hicho wamekiri mbele ya uongozi wa mkoa kuwa wao walikuwa kama kivuli katika eneo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya Sky Sraper Chacha Wangeri amesema kilifanyika na serikali kutwaa eneo hilo ni suala jema kabisa, “Nadhani mkuu wa mkoa alikuwa na nia njema kutaka kujiridhisha nani mmiliki halali wa eneo hilo na leo mkuu wa mkoa ametuthibitishia kuwa sisi sio wamiliki halali na kama kuna mtu anadhani yeye anamiliki ya eneo hilo basi apelike vielelezo ofisini kwake nay eye atakuwa tayari kutengua kauli yake”, Alisema Chacha
Kufuatia Maelekezo ya Serikali, Chacha Wangeri wa Kampuni ya Sky Scraper na Nurdin Suleiman wa kampuni ya Caspian walikabidhi funguo kwa uongozi wa Mkoa walizokuwa wanazishikilia na kisha mkuu wa Mkoa kutangaza rasmi kuwa wanatafuta Mwekezaji makini atakayeweza kuwekeza katika kiwanda hicho.
“Nitangaze tunatafuta mwekezaji Serious nasema Mwekezaji serious aje awekeze sio mababaishaji”, alisema Mongella.
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli imejizatiti katika kuhakikisha nchi inakuwa ya Viwanda na kuweza kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.