RAS BALANDYA AWATAKA WADAU WA MAJI KUWA WAADILIFU
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana amewataka wadau wa usimamizi wa rasilimali za maji kuwa waadilifu na wazalendo ili kuhakikisha huduma hiyo muhimu inasimamiwa na kulindwa.
RAS Balandya ametoa wito huo leo Disemba 19, 2024 wakati akifungua Mkutano wa Jukwaa la mapendekezo ya wajumbe wa Bodi ya Maji ya bonde la ziwa victoria uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa MWAUWASA jijini Mwanza.
Aidha, amewataka wadau hao kuhakikisha wanaendelea kuisaidia Serikali kwenye usimamizi na uendelezaji wa rasilimali hiyo kwa manufaa ya Taifa na kwa kiu kubwa ya kuhakikisha watanzania wanaendelea kupata maji safi na salama.
"Maji hayana mbadala, tutunze rasilimali hii muhimu, kama tujuavyo kuwa hakuna uwezekano wowote wa kupika chakula bila kuwa na maji na mambo mengine mengi hivyo kwa umuhimu huo twendeni tukatunze maji." Amesisitiza Katibu Tawala.
Naye, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Dkt. Renatus Shinhu amebainisha kuwa kikao hicho cha wadau ni cha kisheria katika kupata bodi ya 8 baada ya kuisha rasmi kwa muda wa bodi ya 7 mwezi Disemba 2024.
Aidha, amefafanua kuwa Bodi ya Maji ya Bonde la ziwa Victoria ilipata wajumbe wa bodi ya kwanza mwaka 2000 mara tu baada ya kuanzishwa kwa bodi hiyo chini ya sheria namba 11 ya 2009.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.