RAS BALANDYA AZITAKA HALMASHAURI KUTEKELEZA KWA WELEDI MRADI WA USAID KIZAZI HODARI
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ndugu Balandya Elikana amefungua kikao kazi cha mrejesho wa mradi wa USAID Kizazi Hodari Kanda ya Kaskazini Mashariki unaolenga kuboresha na kuimarisha afya na ustawi wa watoto, vijana na kaya zao walioathiriwa na virusi vya ukimwi na kuzitaka halmashauri zote zilizopitiwa na mradi huu kutekeleza kwa weledi ili kufikia malengo.
Akizungumza leo Novemba 13, 2024 na wadau wa mradi huo wakiwemo wasimamizi wakuu Kanisa la Kilutheri (KKKT) makao makuu kwenye ukumbi mkubwa wa Ofisi ya mkuu wa mkoa, Balandya amesema Serikali inatambua mchango wa wadau wa maendeleo katika kuwapatia huduma bora wananchi, hivyo ni wajibu kuendelea kuwapa ushirikiano.
"Nawapongeza kwa kuvuka malengo mliyojiwekea kutoka idadi mliyojiwekea ya walengwa 44,768 na kufika48,790 sawa na asilimia 109", Balandya.
Vilevile, amezipongeza Halmashauri za Jiji la Mwanza na Sengerema kwa kuingia kwenye kumi bora za zilizofanya vizuri miongoni mwa Halmashauri 184 na kuzitaka nyingine ziige mfano huo.
Awali, akimkaribisha mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba amebainisha wameweka mikakati kwa waganga wakuu wote wa Wilaya kuhakikisha mpango wa afya, lishe, msaada wa kisaikolojia na huduma zote stahiki kwa watoto kuanzia umri wa 0-17 na vijana kuanzia 18-20 vinafanywa vizuri.
Mradi huo wa USAID Kizazi Hodari unatekelezwa katika mikoa 9 ukiwemo Mwanza na malengo ya mwaka 2025 ni kuwafikia walengwa 58165.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.