Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ngusa Samike amefanya ziara ya ukaguzi wa Miradi ya Afya na Vifaa Tiba katika Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema na Misungwi Mkoani Mwanza na kutoa maelekezo ya marekebisho ya haraka.
Akiwa Halmashauri ya Buchosa Katibu Tawala Samike ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Buchosa kuhakikisha Vituo vyote vya Afya vilivyokamilika kuanza kutoa huduma haraka ili kuwapunguzia kutembea umbali mrefu Wananchi.
Aidha ametoa maagizo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,Irene Mukere kuhakikisha Vituo vyote vya Afya vinatumia mfumo sahihi wa Serikali wa ukusanyaji malipo.
"Tusiombe dawa nyingi kutoka Bohari Kuu ya Serikali tofauti na mahitaji, hali hii inasababisha hasara kutokana na dawa kukaa muda mrefu na kuchina"
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa,Julius Mlongo amesema baada ya ziara hiyo ya Katibu Tawala Mkoa sasa ni jukumu letu kuzifanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza katika Miradi ya Serikali ili kuwaletea Maendeleo Wananchi.
Akiwa Wilayani Misungwi katika ziara yake ya ukaguzi wa Huduma za Afya,Vifaa Tiba na utendaji kazi,Katibu Tawala Ngusa Samike ameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo kwa kujenga Hospitali,Vituo vya Afya na Zahanati kwa haraka na usahihi mzuri wa gharama.
Aidha ametoa maagizo ya kutumiwa kila mwezi taarifa ya Maendeleo ya miradi ya Afya na ili kuona mabadiliko chanya ya ziara yake.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi Benson Mihayo amesema wamejipanga kuhakikisha fedha zote zilizotolewa na Serikali upande wa Maendeleo ya Afya wanazisimamia vizuri.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza,Ngusa Samike anafanya ziara ya ukaguzi wa Huduma za Afya na Vifaa Tiba Wilaya zote za Mkoa huo ambapo tayari amezikagua Wilaya tatu za Kwimba,Sengerema na Misungwi na kutoa maagizo ya utekelezaji wa changamoto alizozibaini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.