RAS MWANZA AZINDUA RASMI MRADI WA KUPAMBANA NA UGONJWA WA SELI MUNDU
Karibu Tawala Mkoa wa Mwanza Ndg. Balandya Elikana amezindua rasmi mradi wa kupambana na ugonjwa wa Selimundu na kutoa maagizo kwa Halmashauri zote za mkoa huo kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuutokomeza.
Akizungumza na washiriki wa kikao kazi cha kupambana na ugonjwa huo alhamisi hii kwenye Hotel ya Adden amebainisha kuwa Mkoa wa Mwanza bado una idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na changamoto hiyo hivyo wataalamu wa afya lazima washirikiane kuutokomeza.
"Mkoa wetu kwa mwaka wanazaliwa watoto 1,730 wanaogundulika kuwa na Selimundu, idadi hii siyo nzuri na ndiyo maana Serikali imetoa kipaumbele kwa lkoa huu,"BALANDYA.
Aidha, ameishukuru Wizara ya Afya na TAMISEMI pamoja na wadau wengine kuja Mwanza kutoa elimu kwa jamii kwenye Halmashauri zote 8,hali ambayo italeta matokeo chanya.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Jesca Lebba amebainisha kuwa mradi huo ni hatua kubwa katika sekta ya afya mkoani humo kwani imeshuhudiwa watoto wengi wakiletwa kwenye hospitali za rufaa wakiwa tayari wameathirika.
"Lengo letu kama Mkoa ni kuhakikisha mradi huu unaendeshwa kwa ufanisi ikiwemo uchunguzi wa awali na kutolewa the ba sahihi",Mganga Mkuu.
Washiriki wa kikao kazi hicho ni pamoja na wakurugenzi kutoka Halmashauri zote 8,waganga wakuu wa wilaya pamoja na wataalamu kutoka Hospitali za rufaa Bugando na Muhimbili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.