RC MTANDA AKUTANA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA MARIDHIANO KANDA YA ZIWA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.Said Mtanda amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Jumuiya ya maridhiano Kanda ya ziwa (JMAT) na kuwashukuru kwa kazi nzuri wanayoifanya na kusisitiza bila amani nchini hakuna maendeleo.
Akizungumza na uongozi huo kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi ya mkuu wa mkoa leo Januari 29,2025,Mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha viongozi hao wa dini waliopo katika ziara ya kutembelea miradi ya kimkakati, kuzidi kuhubiri mema yote yanayofanywa na Serikali na inapobidi kukosoa basi nafasi hiyo itumike kwa hekima na busara.
"Wapo baadhi ya watu wanaweza kuwabeza katika hayo majukumu yenu lakini nawasihi msirudi nyuma kwani siyo dhambi kuhubiri ukweli kinachofanywa na Serikali yetu,"Mkuu wa Mkoa.
Mhe.Mtanda amewapongeza viongozi hao kwa uamuzi wa kutembelea miradi ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Meli mpya ya Mv Mwanza na Daraja la JP Magufuli na kujionea lengo la Serikali la kuinua Mkoa wa Mwanza kiuchumi na kuongeza pato la Taifa
"Ndugu zangu hivi sasa tunachangia pato la Taifa asilimia 7 na baada ya miradi hii kukamilika tutafika asilimia 10 hadi 12 kutokana na mkoa wetu kuwa eneo la kimkakati Mataifa jirani yatakuja kwa wingi hapa kufanya biashara,"Mtanda.
Kiongozi wa msafara huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Alhaj Mussa Kalukwenyi amesema wataendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha jamii inaishi kwa amani na ziara yao itazidi kuwaelimisha mipango mizuri ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Viongozi hao ambao ni wenyeviti na makatibu wa mikoa, wanatokea mikoa ya Geita,Mara na Simiyu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.