RC MTANDA AMTAKA MKURUGENZI WA JIJI MWANZA KUSONGA MBELE KAMPENI YA UKUSANYAJI MAPATO
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza Wakili Kiomoni Kibamba kuendelea kukaza msimamo katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi thabiti wa vyanzo vya mapato vya Jiji hilo.
Mhe. Mtanda ametoa tamko hilo alipokuwa akitoa salamu katika kikao cha Baraza maalumu la Madiwani kilichojadili taarifa ya CAG ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo leo Juni 26, 2024.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali haiwezi kukubali kuona vyanzo vyake vya mapato vinachezewa na baadhi ya watu, Mtanda amesema hayupo tayari kuona halmashauri hiyo ikipoteza vyanzo vyake na amemtaka Mkurugenzi kuendelea kusimamia vyema msimamo wake wa ukusanyaji wa mapato kwa maendeleo ya wananchi.
"Kama alivyosema Mkurugenzi kuna watu mnadaiwa na Jiji na wengine mpo humu, hakikisha unasimamia maslahi ya umma na ikiwezekana na huo mkeka wa watu waliokabidhiwa hati za viwanja bila kulipa niletee na mimi nianze nao".Mkuu wa Mkoa
Mhe. Mtanda ameendelea kwa kusema vyanzo vya mapato visiposimamiwa vizuri inaweza kuleta athari kubwa katika uendeshaji wa halmashauri kwani ni mapato kama sivyo basi halmashauri hiyo lazima ife.
Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Mkoa amelipongeza Baraza la madiwani kwa kuendelea kupata hati safi kwa mwaka wa tano mfufulizo kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesbu za Serikali (CAG) na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha hoja zote zilizobaki ambazo hazijajibiwa zinajibiwa kwa wakati.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ametoa muda wa siku mbili yaani mpka kufikia tarehe 28 mwezi wa sita Halmashauri iwasilishe mpango kazi wa utekelezaji wa hoja zilizobaki kwa Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa na namna zitakavyotekelezwa na kuziondoa kabisa.
Akifunga kikao hicho Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Constantine Sima amemuhakikishia Mkuu huyo wa Mkoa kuwa maagizo yote ikiwemo ya usimamizi wa vyanzo vya mapato yeye na wahe. Madiwani watakwenda kuyasimia kwani na wao ni ajenda yao pia.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.