Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wasanii na watayarishaji wa maudhui kutumia Jiji la Mwanza kama eneo la kutengeneza video mbalimbali, akisema mkoa huo una vivutio vingi vya kipekee vinavyoweza kuitangaza Mwanza na Tanzania kwa ujumla duniani kote.

Mhe. Mtanda amesema Serikali ya Mkoa iko tayari kutoa ushirikiano na msaada kwa wasanii na wadau wote wanaotaka kuwekeza katika utengenezaji wa video na kazi za sanaa ndani ya Mwanza.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kikao kifupi kati ya Mkuu wa Mkoa na msanii wa kikazi kipya, Mbwana Yusuph Kilungi maarufu kama Mboso, ambaye yupo Jijini Mwanza kushiriki tamasha la Goodmorning Rocky City Season One litakalofanyika katika Kumbi za Climax zilizopo Rocky City Mall.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ambapo Mhe. Mtanda amempongeza msanii huyo na kuhimiza wasanii kutumia sanaa kama chombo cha kutangaza utalii, utamaduni na fursa zilizopo mkoani Mwanza.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.