RC MTANDA AWAHIMIZA WANANCHI MWANZA KUJITOKEZA KWA WINGI LICHA YA MVUA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amewataka wananchi wa Mwanza kujitokeza kushiriki katika kutimiza haki ya kidemokrasia na kikatiba ya kupiga kura licha ya kuwepo na hali ya mvua na kuwataka hali hiyo isiwatie uvivu.
Mhe. Mtanda ametoa rai hiyo mapema leo Novemba 27, 2024 mara baada ya kushiriki zoezi la upigaji kura na kusisitiza umuhimu wa zoezi hilo kwa kuwa ndio daraja kati ya wananchi na Kiongozi kwa ngazi ya mwanzo kabisa.
"...Wakiona uvivu kuja kupiga kura wakawaachia watu fulani wakapiga kura, wakachagua kiongozi ambae hana sifa na weledi madhara yake ni kwamba wataishi na Kiongozi huyo kwa miaka mitano".
Sasa kuikimbia mvua ya siku moja au kukimbilia matatizo ya kuwa na kiongozi asiye thabiti kwa miaka mitano nini ni bora?, ni bora leo wajitokeze kupiga kura kwa muda mfupi kisha waendelee na shughuli zao. Ameongeza RC Mtanda.
Aidha Mkuu huyo wa Mkuu huyo wa Mkoa amesema katika Mkoa wa Mwanza wamekubaliana kuwa Kiongozi atakayetangazwa ni yule
atakaeshinda.
Zoezi la upigaji kura linaendelea na inatarajiwa kufungwa rasmi saa kumi jioni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.