Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda kupitia mkutano alioufanya na Waandishi wa Habari ametoa shukrani kwa makundi mbalimbali ya Viongozi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Mwanza kwa ushiriki wao katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mkoani Mwanza jini 19 – 21 2025.
Mkuu wa Mkoa amesema ziara ya Rais Dkt. Samia Mkoani Mwanza imekuwa ya mafanikio makubwa kutokana na ushiriki wa Viongozi wa Serikali, Dini, Chama cha Mapinduzi, Makundi mbalimbali kama vile Maafisa Usafirishaji, Machinga na wafanya biashara, walijitokeza kushiriki kikamilifu katika mapokezi na ziara nzima.
“Kwa niaba ya Serikali Mkoani Mwanza nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mwanza, kwa ujumla mimi kama Mkuu wa Mkoa nimeridhika na ziara ya Rais kama ilivyokuwa imeandaliwa”. Mhe. Mtanda.
Adha, Mhe. Mtanda amewashukuru sana wananchi wa mkoa wa mwanza kwa mwitikio mkubwa na hamasa kubwa lakini pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kufanya kazi kubwa ya uzinduzi wa daraja, maji na mkutano mzuri wa sungusungu.
“Kwenye mradi wa maji butimba tunawashukuru sana Taasisi na wizara ya maji lakini pia Viongozi wa Wilaya ya Nyamagana na wananchiwa Nyamagana kwa kujaa kwa wingi”. Amesema.
Kadhalika amewapongeza Viongozi na wananchi wa Wilaya ya Magu kwa kufanikisha Tamasha la Utamaduni la bulabo.
Tunawashukuru kwa ushiriki wao na tunaendelea kuomba ushirikiano wao sio tu kwa ziara ya Rais hata kwa viongozi wengine watakaoweza kuja katika Mkoa wa Mwanza maana picha na taswira tulioonesha imeleta matumani kwamba umoja, mshikamano na upendo umetawala mwanza. Amesema Mkuu wa Mkoa.
Kabla ya kuhitimisha mkutano huo Mhe. Mtanda ametoa pongezi pia kwa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mwanza kwa mchango wao mkubwa sana katika kuhabarisha na kuhamasisha umma kushiriki ziara ya Mhe. Rais.
“Kwa hiyo ninawapongezeni sana kwa ushiriki wenu, mlitoa habari kwa usahihi na kwa wakati, kazi iliyofanyika ni kubwa sana kwa hiyo tunawashukuru mno”.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.