RC MTANDA AZINDUA MRADI WA MAJI KABILA, WANANCHI ZAIDI YA 11, 000 KUNUFAIKA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo Juni 13, 2024 amezindua mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya Tshs. Milioni 205 uliojengwa kwa ushirikiano baina ya SBL na RUWASA unaotarajiwa kunufaisha zaidi ya watu 11000 kutoka kwenye vijiji vya N'gwamagoli na Kabila.
Akizungumza na wananchi baada ya kuzindua mradi huo Mhe. Mtanda ameishukuru Kampuni ya Serengeti Breweries na AFRIcai kwa kutoa Tshs. 180,274,000 na kushirikiana na RUWASA (zaidi ya Bilioni 25) waliotekeleza mradi uliohusisha vituo vya kuchotea maji 13, mtandao wa mabomba KM 6.3 pamoja na tangi la lita 90,000.
"Mkoa wa Mwanza umetenga jumla ya Tshs. 146,315,299,905 katika mwaka 2023/24 - 2024/25 ambapo Wilaya ya Magu pekee imetengewa jumla ya Tshs. 17, 017,927,019 ili kukamilisha miradi 7 inayoendelea kutekelezwa." Amesema, Mkuu wa Mkoa.
RC Mtanda amefafanua kuwa ujenzi wa mradi huo muhimu kwa wananchi ni utekelezaji wa agenda ya Rais Samia katika kusudio lake la kumtua mama ndoo kichwani na utelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2025 inayoitaka Serikali kufikisha huduma ya maji vijijini kwa 85% au zaidi hadi kufikia 2025.
"Serengeti Broweries Limited imetumia zaidi ya Tshs. Bilioni 2.5 2023/24 kwenye uchangiaji wa miradi ya huduma kwa jamii ikiwa ni katika kuhakikisha inasaidia kuondoa adha ya upatikanaji wa maji safi na salama na kupambana na ukame unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi hususani vijijini." Mkurugenzi Mtendaji SBL, Dkt. Obinna Anyalebechi.
Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Joshua Nathari amewataka wananchi kulinda miundombinu ya mradi huo ili lengo la kuongeza upatikanaji maji pamoja na kupunguza umbali na muda wa kufuata maji lidumu kwa muda mrefu na kusaidia kumaliza kero ya maji moja kwa moja.
Naye Meneja wa Wakala ya Maji vijijini (RUWASA) Mkoa wa Mwanza Mhandisi Godfrey Sanga amesema Januari 2024 ujenzi wa mradi ulianza na Aprili 2024 umekamilika na kuna matarajio ya kufikisha asilimia 86 kutoka 71 za usambazaji maji vijijini kwa wananchi wa wilaya ya Magu.
"Tulikua tunasumbuka sana na huduma za maji lakini kwa sasa usumbufu wote umeisha kutokana na Rais Samia kutupendelea maana kwenye vitongoji vyetu vitano kati ya sita sasa tumepata naji safi tunaomba mtupelekee huduma hii kwenye kijiji hicho cha Ilambu." Mwenyekiti wa Kijiji cha Kabila, Mwajibu Boniface.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.