RC MTANDA KULIVALIA NJUGA KERO YA VIJANA WAHALIFU WA MITAANI WATAKAPO THIBITIKA
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema atajiridhisha kupitia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza kuhusu uwepo wa Vijana wa mtaani wanaojihusisha na masuala ya uhalifu na endapo itathibitika kuwa ni kweli ataendesha operesheni ya kuwakamata Vijana hao na ameahidi kuwapeleka katika nyumba za kutibu watu walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya (Sobber House).
Hayo ameyasema leo Juni 11, 2024 alipokuwa mubashara katika kipindi maalumu kupitia runinga ya Mahaasin TV, wakati akijibu swali aliloulizwa kuhusu kuzuka kwa wimbi la Vijana wanaojihusha na uhalifu hasa katika maeneo ya mjini.
Mhe. Mtanda amesema hawezi kulitoleaa ufafanuzi kwa sababu bado hajapata taarifa hizo na kwa kuwa ndio mara ya kwanza kusikia basi anahitaji kujiridhisha kupitia vyombo vya kisheria.
Akiendelea kutoa ufafanuzi Mhe. Mtanda amesema ana uzoefu mkubwa katika kushughulika na masuala hayo ya kiuhalifu na kwa uzoefu wake amesema kuwa vijana wengi wanaofanya uhalifu wanakuwa ni waraibu wa matumizi ya dawa za kulevya.
"Kwa uzoefu wangu vijana wengi wamekuwa wahalifu kutokana na uraibu wa madawa ya kulevya hivyo endapo nitawakamata basi hakuna haja ya kuwapeleka polisi maana bongo zao tayari zimekwisha kuathirika na dawa hivyo sobber House ndio mahali sahihi kwao".Mkuu wa Mkoa.
Aidha RC Mtanda ambaye anafanya ziara kwenye vyombo vya habari Mwanza, amesema suala hilo atalifuatilia kwa ukaribu na atatoa majibu mara tu atapojiridhisha kutoka kwa Kamada wa Polisi Mkoa wa Mwanza.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.