Amebainisha hayo leo Julai 19, 2022 Jijini humo wakati akifungua Mafunzo ya Viongozi wa Dini ya kujengeana uwezo katika kulinda na kudumisha amani yaliyoandaliwa na Kamati ya Amani.
"Tuendelee kushikamana kwa pamoja na msingi huu umezidi kuwa chachu ya Maendeleo miongoni mwa Jamii na hata kunapotokea sintofahamu utatuzi unapatikana haraka kutokana na msingi imara tulioujenga" amesema Mkuu wa Mkoa
Aidha, amewakumbusha Viongozi hao kuendelea kumuombea Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kuisimamia na kuiongoza vyema nchi yetu kwani jukumu alilonalo ni zito na linahitaji maombi ya mara kwa mara.
Awali akizungumzia mafunzo hayo Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo Askofu Charles Sekelwa amebainisha huo ni muendelezo wa majukumu yao ya kuhakikisha Viongozi wanapata msingi mzuri wa kuendeleza amani katika maeneo yao.
Naye, Sheikh Hassan Kabeke ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani Mkoa amesema Kwa kutambua umuhimu wa Amani na Maendeleo miongoni mwa Jamii wataendelea kushirikiana na Serikali katika shughuli za maendeleo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya kujenga Amani ambao pia ni wawezeshaji wa Mafunzo hayo Canon Goda amesema Taasisi hiyo imekuwa mstari wa mbele kutoa elimu hiyo hapa nchini kwa muda mrefu kabla na baada ya kusajiliwa na kumekuwa na matokeo chanya.
Mafunzo hayo ya siku mbili yamewashirikisha Viongozi wa Dini kutoka Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa ukiwemo na Shinyanga.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.