Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe Mhandisi Robert Gabriel amewahakikishia wananchi wa Makaazi ya Milimani Mkoani humo kuwa wapo salama kwenye makazi yao na hakuna mtu anayeweza kuwaondoa kwenye maeneo hayo kinyume cha sheria.
Amebainisha hayo leo Juni 15, 2022 wakati akizungumza na wakaazi wa Kata ya Igogo na Pamba alipofika kusikiliza kero za wananchi hao na kukagua maendeleo ya mradi wa kuondoa maji taka kutoka kwenye makazi hayo.
"Maeneo yapo salama, mtu aliyeko juu mlimani anafanana na aliye chini wote ni sawa kwa mujibu wa sheria na ukiwa na leseni ya makazi au hati yako akija mtu analitaka eneo lako basi akuachie mahela na hakuna mtu wakukupokonya, kukufukuza wala kukudhulumu," amesema.
"Mhe Rais amefanya mambo makubwa sana kama mnavyoona huko juu kuna matenki yanaondoa maji taka na kuyaleta kwenye mfumo mkubwa huku chini na kila mtu mwenye eneo huko juu anapimiwa ardhi na kupewa leseni ya makazi ili kumhakikishia usalama wa eneo lake." Mkuu wa Mkoa amesisitiza..
"Ndugu zangu serikali imewekeza zaidi ya Bilioni 2.6 kwenye mradi wa miundombinu ya Maji Taka na unahusisha pia njia za kupanda na kushuka wananchi ambazo nimewaomba wauboreshe kwa kuweka kingo kwenye njia hizo ili wakaazi wapate kuwa salama zaidi." Mkuu wa Mkoa amesisitiza.
"Kwa upande wa kata ya Igogo na zingine tano tuna mradi wa kutambua vipande vya ardhi na kuyatambua rasmi ikiwa ni kuboresha maeneo ya vilima kwahiyo wananchi elfu 12 tumewatambua na tunawapatia leseni za makazi na wizara ya ardhi imewezesha na taarifa zinatumika kwenye mfumo wa anuani za makazi na zitatumiwa kwenye Sensa ya Watu na Makazi. Kamishna wa Ardhi Mkoa, Elia Kamihanda.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mwanza, Mhandisi Martha Chuwa amesema kwa kushirikiana na serikali wanatekeleza mradi wa Maji Taka na safi na kaya zipatazo 393 kwa upande wa Igogo na maeneo mengine ambapo kwa ujumla Mradi huo umegharimu bilioni 2.6 na Umeshaanza kutekelezwa.
"Namshukuru sana Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuboreshea makazi ya wakaazi wa milimani na tumeona pale mradi wenye zaidi ya Bilioni mbili, nawahakikisha wananchi wangu hakuna atakayehamishwa." Mhe Diwani wa Kata ya Igogo Mhe Ramadhan Mahila.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.