• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

SERIKALI IMEENDELEA KUKUSANYA MAONI YA MAREKEBISHO SERA YA MAMBO YA NJE YA MWAKA 2001:NAIBU WAZIRI MBAROUK

Posted on: April 19th, 2024

SERIKALI IMEENDELEA KUKUSANYA MAONI YA MAREKEBISHO  SERA YA MAMBO YA NJE YA MWAKA 2001:NAIBU WAZIRI MBAROUK


Serikali imeendelea kukusanya kukusanya maoni ya Watanzania kuhusu marekebisho ya sera ya mambo ya Nje iliyotungwa mwaka 2001 na kuanza kutumika 2004 ambayo imekuwa haitoi fursa pana katika majukwaa ya kimataifa na ndani ya nchi.

Akizungumza kuhusu sera hiyo leo Aprili,19 2024 kwenye ukumbi wa mikutano,Gold Crest Naibu Waziri wa Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe:Mbarouk Nassoro Mbarouk wakati wa kongamano la tano Jijini Mwanza amebainisha maoni hayo wanaamini yatakuwa na mchango mkubwa wa kuleta mageuzi ya kimaendeleo.

 “Tanzania kama yalivyo Maataifa mengine inakabiliwa na fursa na changamoto katika ushiriki kwenye majukwaa ya kanda na kimataifa hivyo kuwa na sera madhubuti ni muhimu ili kutumia fursa  zinazotokana na ushiriki wa nchi zetu kwenye majukwaa hayo ikiwa pamoja na kukubaliana vyema na changamoto zinazojitokeza”

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe:Hassan Masala aliyekaimu nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, amesema Mkoa wa Mwanza ni kitovu cha biashara kwakuwa imezungukwa na nchi jirani kama Rwanda na Burundi vivyo ni muhimu kwa mkoa huo kutoa maoni na mapendekezo kuhusu marekebisho ya sera mpya ya mambo ya nje ya mwaka 2001.

“Tuna mkoa wa kimkakati ambao nchi za maziwa makuu unautegemea katika shughuli za kiuchumi zikiwemo za uvuvi,madini na usafirishaji" Mkuu wa Wilaya

"Huu uraia pacha binafsi sioni kama una mashiko japo nasikia ukipigiwa sana debe,tujivunie utaifa wetu,mtu akienda nje basi aamue abaki na utaifa wake au aombe huko alipo",Masala Kulangwa,Mwenyekiti Baraza la Wazee.

"Nashauri huu uteuzi wa mabalozi uanzie ngazi ya chini kwa wananchi kushirikishwa ili kuwepo na uwazi na kumpata mtu sahihi atakaye kwenda kuiwakilisha nchi yetu," Irine Joseph,mwana zuoni,SAUT

"Vyombo vya habari nashauri viongezewe uwanda mpana wa kufanya kazi zake hasa kutokana na utanda wazi uliopo sasa,naipongeza Serikali kwa uamuzi huu wa marekebisho haya",Issa Hussein,mtoa maoni.

Baadhi ya wadau walioshiriki kutoa maoni ni wanasiasa,viongozi wa Baraza la wazee ,wakuu wa Taasisi za umma,wana zuoni,  na wahadhiri.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.