• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

TAMISEMI ilivyotumia Wiki ya Kitaifa ya Usalama Barabarani Mkoani Mwanza kwa kutoa huduma mbalimbali kwa jamii

Posted on: March 22nd, 2023


Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na idara na sekta mbalimbali ambazo ziko chini ya wizara hiyo wameadhimisha wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyofanyika Kitaifa Mkoani Mwanza kwa kutoa huduma tofautitofauti kwa wananchi ikiwemo kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali, kukusanya damu, chanjo ya Uviko 19 na kutoa elimu jinsi ya kujikinga na ajali.

Maadhimisho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yalifanyika Mkoani Mwanza katika Uwanja wa Furahisha uliopo Wilaya ya Ilemela kuanzia Machi 14 hadi 17, 2023 yakiwa na Kauli Mbiu isemayo Tanzania bila ajali inawezekana-Timiza wajibu wako.


Idara na Sekta zilizoshiriki kutoa huduma hizo ni Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure, Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando(BMC), Hospitali ya CF, Msalaba Mwekundu(RED CROSS) Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani  (UNICEF) na Ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Damu Salama.

Akizungumzia huduma hizo,  Mratibu wa Huduma za Maabara na Damu Salama Mkoa wa Mwanza, Juma Shigella, alisema Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando(BMC) na Hospitali ya CF  zilifanya vipimo vya magonjwa mbalimbali kwa wananchi, RED CROSS) ilitoa  elimu kwa wananchi  jinsi ya kujikinga na ajali, UNICEF iliratibu utoaji wa chanjo ya Uviko 19 na Ofisi ya Kanda ya Ziwa ya Damu Salama kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure walifanikiwa kukusanya jumla ya chupa 35 za damu.

“Tuliona tutumie Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kwa ajili ya kukusanya damu kwa hiari kutoka kwa wananchi ambao wanatembelea mabanda yetu ingawa maadhimishio haya yanaenda sambamba na utoaji wa elimu lakini huduma ya damu salama ni muhimu sana kwa sababu ajali nyingi zinapotokea watu wengi wanapoteza damu hivyo ili kuokoa maisha yao huhitaji damu,  tuliona kuna umuhimu wa kukusanya damu katika mkusanyiko huo,”alisema Shigella na kuongeza

“Tunaishukuru sana Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kama viongozi wetu ambao ndiyo dira yetu katika utoaji wa huduma za afya wamekuwa nasi katika kipindi cha wiki nzima ya maadhimisha haya  tumetoa huduma za upimaji wa magonjwa mbalimbali kwa wananchi ikiwemo  Virusi vya Ukimwa(VVU) na kisukari.

“Pia tumetoa elimu kuhusiana na lishe bora kwa kuzingatia makundi ambayo yanahitajika mwilini ili kupunguza vyakula ambavyo havihitajiki kwa ajili ya afya, namna ya kujikinga na ajali, namna ya kujikinga na magonjwa mbalimbali na   upimaji wa macho,”alisema Shigella.


Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.