Utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa barabara ya Makongoro hadi uwanja wa ndege unatarajia kukamilika mei 2 mwaka huu.
Mkataba wa ujenzi wa barabara hiyo uliosainiwa April 18 mwaka 2017 na M/s Nyanza Road Work Ltd ambapo gharama za mradi ni shilingi 9,542,701,531.96 unaosimamiwa na kitengo cha ushauri wa kihandisi cha wakala wa barabara TECU.
Akizungumza kwenye kikao cha pili cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mwanza kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Meneja wa TANROADS Mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya kilichofanyika jana mkoani hapa alisema, hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 74 ambapo ujenzi wa barabara hiyo kuanzia Mwaloni-Furahisha na Pasiansi hadi uwanja wa ndege upo katika hatua mbalimbali.
Mhandisi Rubirya alisema, uwekaji wa tabaka la lami ngumu imefikia urefu wa km 2.2, lami ya awali urefu wa km 2,9, tabaka la mawe yaliyosagwa urefu wa km 2.9,tabaka la msingi wa barabara km 3.1 na ujenzi wa daraja la Ilemela umekamilika kwa asilimia 90, hivyo utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kukamilika mei 2 mwaka huu.
Hata hivyo alisema, usanifu wa kina wa upanuzi wa daraja la Mabatini lililopo barabara ya Mwanza- Musoma utakamilika mwezi aprili mwaka huu na kazi inaendelea inayofanywa na Mkandarasi Mshauri M/s Advance Engineering Solution kwa gharama ya milioni 242,574.
Hatua hii ni kutokana na kuepo tatizo la mafuriko kwa muda mrefu kwenye daraja hilo pindi mvua zinaponyesha na kusababisha maji kupita juu ya barabara kwa kuwa na midomo midogo ya kupitishia maji.
Aidha, ofisi ya Meneja mkoa kwa kushirikiana na wahandisi washauri wataendelea kusimamia utekelezaji wa miradi yote ili ikamilike kwa wakati kama ilivyopangwa hivyo kwa kuiwezesha ofisi yao kutekeleza majukumu ya kujenga na kusimamia matengenezo ya barabara kama ilivyoidhinishwa katika bajeti ya wizara yao wanashauri fedha zitolewe kwa wakati.
Kwa upande wake Mratibu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Mwanza Francisco Magoti alisema, dhima yao ni kupanga,usanifu,ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara za vijijini na mijini kwa kuzingatia ufanisi wa gharama kwa ajili ya maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi nchini.
Alisema, TARURA ina mtandao wa barabara wenye urefu wa km 4891.56 kwa Halmashauri zote za mkoa huo,ambapo barabara ya lami km120.41,barabara ya mawe km 8.537, barabara ya zege km 2.51, barabara za changarawe km 1525,673 na barabara ya udongo km 3235,22.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela John Wanga aliomba kipande kitakacho baki cha barabara ya Buswelu hadi Igoma nacho kijengwe kwa kiwango cha lami, ili kuleta taswira nzuri na wananchi kufanya shughuli za uchumi kwa urahisi baada ya kukamilika kwa mradi wa barabara ya Buswelu kupitia Kiseke mpaka Sabasaba ambao unakaribia kuanza mei, huku Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mary Tesha aliwaomba TARURA kuendelea kushirikiana na wakuu wa wilaya na wabunge katika kutekeleza majukumu yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.