• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • ununuzi na Ugavi
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Sheria
  • Wilaya
    • Ilemela
    • Nyamagana
    • Magu
    • Misungwi
    • Kwimba
    • Sengerema
    • Ukerewe
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Jiji la Mwanza
    • Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
    • Hamashauri ya Wilaya ya Magu
    • Hamashauri ya Wilaya ya Sengerema
    • Hamashauri ya Wilaya ya Misungwi
    • Hamashauri ya Wilaya ya Kwimba
    • Hamashauri ya Wilaya ya Ukerewe
    • Hamashauri ya Wilaya ya Buchosa
  • Fursa za uwekezaji
    • Miundombinu ya Umwagiliaji na kilimo cha mkataba
    • Kilimo
    • Madini
    • Sekta ya Huduma
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa vyombo vya habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya video

Wakurugenzi Waapishwa kuaimamia Uchaguzi

Posted on: August 5th, 2019

Wakurugenzi wa Halmashauri  na maofisa mbalimbali wa wateule  wameapishwa mkoani Mwanza   kwa ajili ya mchakato wa kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa huku wakionywa kwamba atakayekiuka kiapo ataadhibiwa kwa sheria ya  usalama wa taifa.

Akizungumza na wakurugenzi hao kabla ya kuwaapisha, Hakimu kutoka Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Bonaventure Lema, alisema yeyote alikayeapa na kutoa siri kwa mtu asiyehusika atachukuliwa hatua za kisheria kwa kutumikia jela zaidi ya miaka  20 kwa kutumia sheria ya kutunza siri ya usalama wa taifa hata akiwa amestaafu.

“Kazi yangu iliyonileta hapa ni ndogo tu ya kuwaapisha na kurudi katika eneo langu la kazi kuendelea na majukumu ya kila siku  wala sihitaji kupata mafunzo yenu, baada ya kiapo hiki naomba kama wewe ni mfuasi wa chama chochote cha siasa tambua kiweke pembeni.

“Baada ya kukamilisha shughuli iliyosababisha  ule kiapo  ni ruksa kurudia chama chako na kuendelea na uanaharakati, naomba  kila mmoja anieleze  maana ya siri au nielezeni siri ya watu wawili ni siri,”alihoji huku wajumbe hao wakimjibu sio siri.

“Naomba niwaambie siri ni jambo lolote ambalo hupaswi kulisema kwa mtu mwingine, hiyo ndiyo siri sasa baada ya kuapa hapa hatutarijii tena mtu anakwenda kumwambia mtu mwingine kisha anamwambia hiyo ni siri, hatua zitachukulia na haijalishi kama umestaafu, sheria za kutunza siri ya  usalama wa taifa zitachukua mafasi yake,”alisema.

Awali, akifungua  simina ya mafunzo kwa wakurugenzi hao na maofisa wengine wateule, Kamishna wa Tume ya Uchaguzi nchini (NEC), Asina Omar aliwaonya  mawakala wa vyama vya siasa kuingilia  utendaji kazi ya watalaam badala yake wapaswa kuwapo katika vituo ili kushuhudia namna shughuli inavyofanyika kwa haki.

Omar alisema mawakala anaruhusiwa kuwapo katika maeneo ya vituo lakini si kwa ajili ya kufanya  kazi  ambayo hawana uzoefu wala mafunzo, hivyo wanapaswa kutambua wao wafanye kazi waliyoagizwa na vyama vyao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

Kuhusu  mafunzo  kwa wakurugenzi na maofisa , alisema lengo ni  kuwaongezea uelewa na matumizi ya  ya mashine ya BVR kit itakayotumika katika kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura.

Alisema uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Mkoa wa Mwanza linatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 13 hadi 19 ambapo aliwataka watumishi wote  wakiwamo wakurugenzi, maofisa uchaguzi wa halmashauri na watalaamu wa Tehema kutimiza wajibu na majukumu yao ipasavyo na kutoa elimu kwa waandikishaji.

“Kila mmoja atimize wajibu wake na mnapaswa kuelewa hatutaki tena kufanya shughuli hii kwa mazoea, wapo wenye uzoefu na shughuli hii hawapaswi kupuuza kwa kigezo wanajua hapana, hakikisheni mnafuatilia hatua kwa hatua, toeni elimu pale unapona inahitajika.

“Mjiamini kama watu mliopewa mafunzo lakini kikubwa ni kuzingatia sheria na miongozo iliyowekwa, jaribuni kuonyesha kujitambua na kutambua miundombinu mtakayokwenda kufanyia kazi, wale wa tehema hakikisheni linapojitokeza suala linalowahusu tatueni haraka, kama lipo  linahitaji sisi kuhusika tujulishane haraka,”alisema.

Matangazo

  • Tangazo la kukutana na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa shida mbalimbali. January 08, 2025
  • TANGAZO LA NANENANE TAREHE 8.8.2025 January 08, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • UZALISHAJI ZAO LA PAMBA WAONGEZEKA- MSIGWA

    May 03, 2025
  • DARAJA LA KIGONGO-BUSISI KUANZA KUTUMIKA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA.

    May 02, 2025
  • SERIKALI YAANIKA TAKWIMU ZA MAENDELEO YA UTUMISHI YALIYOPATIKANA MWANZA

    May 01, 2025
  • MAKUNDI MAWILI YA MWISHO YALIYOFANYA ZIARA HIFADHI NA JNHPP YAWASILISHA NENO LA SHUKRANI KWA RAS BALANDYA

    April 29, 2025
  • Angalia zote

Video zinazotembea

Siku 365 za Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan Mwanza
video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu ya Ugonjwa
  • FFARS User Guidelines
  • Miongozo ya mfumo wa bajeti na Mipango
  • Makusanyo ya Ndani ya Halmashauri za Mkoa wa Mwanza
  • PReM
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
  • Opras fomu
  • OFISI MTANDAO

Viunganishi Linganishi

  • Tovuti ya Ikulu
  • Utumishi
  • Tamisemi
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive

    S.L.P: 119, Mwanza.

    Simu: 028-2501037

    Simu ya Mkononi: 028-2501037

    Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.