WANANCHI WA LUCHELELE WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAJENGEA BARABARA YA LAMI
Wananchi wa kata ya Luchelele jijini Mwanza wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea barabara ya Luchelele, Bismark, Mwananchi Mahina Kati na Buhongwa Bulale - Mwasonge kwa kiwango cha lami kwani itarahisisha usafirishaji.
Akiongea kwa niaba ya wananchi, Diwani wa Kata ya Lichelele Mhe. Vicent Tega amesema wananchi wa maeneo hayo wamepata faraja sana kuona ujenzi wa barabara hizo muhimu na maarufu kwa usafirishaji wa vyakula na biashara kwani siku za nyuma walikuwa wakipata adha.
Hayo yamejiri leo 17 Julai 2024 wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alipotembelea eneo la Luchelele kukagua ujenzi wa Barabara zenye urefu wa Kilomita 1.40 zinazotekelezwa na Mkandarasi M/s Jassie &Company Limited kwa gharama ya Tshs. 1,050,000,000.
Akizungumza kwenye ukaguzi huo Mhe. Said Mtanda Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amewataka wananchi kulinda barabara hizo na TARURA kuhakikisha wanasimamia ukamilishaji na ulinzi wa miundombinu hiyo ambapo kwa sasa umefikia asilimia 90.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.