Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB) ametoa rai kwa vijana na wananchi kwa ujumla kuipenda Nchi na kutunza mali ambazo zinazunguka maeneo yao kwa ujumla.

Rai hiyo imetolewa leo Disemba 5, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Magu Kata ya Kisesa mara baada ya kukagua baadhi ya maeneo yaliyo haribiwa na vurugu zilizotokea tarehe 29, Octoba 2025 katika Mkoa wa mwanza.

Aidha, amesema serikali itaendelea kuisimamia na kuitekeleza miradi ya maendeleo huku akiutaka uongozi wa Mkoa kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa huu.

"Vijana tusirubuniwe hii ofisi mlioichomamoto sio mali ya mtendaji wa kata imejengwa kwa fedha yenu wenyewe wananchi wa wilaya ya kisesa na magu kwa ujumla". Amesisitiza hayo wakati akikagua ofisi ya kata ya Kisesa iliyochomwa moto.

Halikadhalika, amebainisha malengo ya serikali ya kutoa ajira elfu 12 katika sekta za afya na elimu, kuanzisha programu ya bima ya afya kwa wote nchini na kutolipa fedha kwa ajili ya kutoa maiti hospitali ndani ya siku 100.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda alimjulishwa Waziri Mkuu kuwa Kisesa ilikua kitovu cha vurugu siku ya uchaguzi kwani vijana waliqnzia hapo kuharibh mali na baadae kusambaa katika maemdeo mengine.

Vilevile Mhe. Mtanda amesema uharibifu iliofanyika katika kata ya kisesa umewakosesha wananchi huduma za kikodi mabaraza ya ardhi mikopo ya vikundi na huduma za kimahakama.

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.