Benki ya Posta Tanzania (TPB) yatoa msaada wa tani 20 za saruji kwa hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando ili kuchangia ujenzi wa wodi ya wagonjwa wa saratani .
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella ,Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki ya TPB Sabasaba Moshingi alisema Benk ya TPB inatenga fedha Kila mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii ambapo kwa mwaka jana walitenga million mia tatu kwa ajili ya kusaidia jamii kwa mwaka huu .
Alisema wameamua kutoa msaada huo ambao utasaidia juhudi za Bugando na watu wa Mkoa wa Mwanza kwani hospital hiyo ni muhimu inahudumia mikoa 8 ya kanda ya ziwa na Magharibi yenye watu zaidi ya million 18.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospital ya Kanda ya Rufaa ya Bugando Dr.Fabian Massaga alisema Kanda ya Ziwa inaongezeko kubwa la idadi ya wagonjwa wa saratani linaonyesha jinsi ugonjwa huo ulivyo changamoto katika jamii na eneo lote la kanda ya ziwa,hivyo wanaishukuru Benki hiyo kwa kuwashika mkono ili kufanikisha ujenzi huona wataendelea kuhamasisha wadau wengine kuendelea kuchangia ili tufanikishe ujenzi huu.
Alisema mradi huo ulianza mwaka jana na ukitarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja na utagharimu billion 5.4 ambapo billion 1 ni kwa ajili ya gharama za ufundi , billion 4.1 kwa ajili ya vifaa na million 200 kwa ajili ya Mhandisi Mshauri,pia wodi hiyo. itakayokuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 120 kwa wakati mmoja,vyumba vya kuonea wagonjwa na kutolea dawa.
"Naishukuru serikali kwa kutoa billion 1 kwa ajili ya kutuwezesha ambapo hadi sasa mradi huo umewagharimu billion 1.5 ." alisema.
Kwa upande wake Mkoa wa Mwanza John Mongella alisema juhudi hizo ni za serikali kujaribu kuboresha kwa kiwango kikubwa huduma za afya kwani bila kuwa na watu wenye afya timamu yote yanayozungumziwa ya kutuletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja, familia , jamii ,mkoa na nchi hayatawezekana .
Alisema jamii itakapokuwa na afya juhudi za maendeleo zitakuwepo kutokana na Bugando kuanzisha mradi huo wakutoa tiba za juu za saratani hivyo wadau wajitokeze
" Leo tumeona Benk ya TPB mwaka jana walitoa msaada na mwaka huu wamerudi tena kutoa msaada nawashukuru sana kwa sababu haijatoa msaada huo kama wamepoteza bali wamewekeza kwenye afya za wananchi ambao ndio soko lao" alieleza Mongella.
Aliongeza kuwa tangu alipoingia madarakani Rais Samia Hassan Suluhu ni muda mfupi ambazo hivi karibuni alitoa billion I kwa ajili ya ujenzi huo hivyo anashukuru kwa kutambua mchango wa wodi hiyo hivyo watanzania wamuunge mkono kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuiwezesha nchi yetu kwenda kwa kasi zaidi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya changizo la mradi wa ujenzi wodi ya saratani Bugando Dr Pastory Mondea alisema wanatambua mchango wa Benk hiyo hivyo walitoa Cheti cha kushukuru na kutambua mchango wao pia aliwaombaa wadau wote watakaoguswa na ujenzi huu ambao ni muhimu kwa jamii wawaauunge mkono .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.