Waziri wa Kilimo Dkt.Charles Tizeba(Mb) amewaasa viongozi wa vyama vya Ushirika kuangalia changamoto mbalimbali zilizopo katika vyama hivyo na kuzitatua ili viwe imara na vyenye tija kwa wananchi wote.
Awali akifungua Kongamano la ushirika lililofanyika katika viwanja vya Furahisha Mkoani Mwanza Mhe. Tizeba amesema kuwa hivi sasa kama nchi inabidi kujitafakari na kuweza kujua sababu zinazopelekea watu wasijiunge na vyama vya ushirika.
"Tupo watu miliono 54 lakini wanaushirika wa vyama vyote hawafiki milioni nne hii ni chini ya 10%,sasa tuanzie hapo katika kutafakari kitu gani kimetokea watu hawajiungi tena katika ushirika"alisema Tizeba.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainabu R. Telack ambaye ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema, kupitia Ushirika tutegemee manufaa makubwa kwani katika nchi yetu Ushirika ndiyo mkombozi pekee kwa wananchi.
"Kongamano hili ndilo pekee ambalo wanaushirika wanakwenda kujadili jinsi ya kuimarisha vyama vya ushirika maana ni tegegemeo pekee la wa kulima, "alisema Telack.
Maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani huazimishwa kila Jumamosi ya kwanza ya mezi julai na kauli-mbiu ya mwaka huu ni "Ushirika kwa ulaji na uzalishaji endelevu wa bidhaa na huduma".
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.