Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza CP.Clodwig Mtweve ametoa Taarifa ya Matokeo ya Mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE 2017) Katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
CP. Mtweve amesema kuwa Mkoa wa Mwanza umepata ufaulu wa wa asilimia 77.3 ambapo kati ya watahiniwa wote 70368 waliofanya Mtihani huo ni watahiniwa 54367 ndio waliopata alama za ufaulu yaani kati ya alama 100 mpaka alama 250.Ameongeza kuwa kati ya watahiniwa waliofaulu wavulana ni 27971 na wasichana ni 26396 hali iliyopelekea Halmashauri zote 8 kupata za Mkoa wa Mwanza kupata ufaulu zaidi ya asilimia 50.
Aidha ufaulu katika Halmashauri zilizopo Mkoa wa Mwanza ni kama ifuatavyo ambapo Halmashauri ya Jiji la Mwanza 88.7% ,Ilemela 87.5%,Buchosa 85.8%,Sengerema 82.3%,Misungwi 79.4%,Kwimba 73.7%,Magu 71.6% na Ukerewe 50.7%.
Ufaulu wa Shule 10 Bora Kimkoa kundi la Watainiwa zaidi arobaini (40+) Shule ya Alliance imekuwa ya kwanza Kiwilaya na Mkoa ya Kwanza wakati Kitaifa imekuwa ya tatu, Mugini imeshika nafasi ya kwanza kiwilaya wakati Kimkoa imekuwa ya pili na Kitaifa imekuwa ya 15.Kazungu imekuwa uya 1 kiwilaya ya 3 kimkoa na imeshika nafasi ya 25 Kitaifa.Shule ya Msingi Nyamuge imekuwa ya 1 Kiwilaya ya 4 Kimkoa na imeshika nafasi ya 30 Kitaifa.
Shule ya Msingi Tulele imeshika nafasi ya 2 Kiwilaya ya 5 Kimkoa na Kitaifa imeshika nafasi ya 31. Lake View imekuwa ya 3 Kiwilaya ya 6 na Kitaifa ni ya 45. Kimiza imekuwa ya 1 Kiwilaya ya 7 katika Mkoa na 58 Kitaifa. Buswelu imekuwa ya 2 Kiwilaya ya 8 Kimkoa na Kitaifa imeshika nafasi ya 62. New Alliance imekuwa ya 2 Kiwilaya ya 9 Kimkoa na imeshika nafasi ya 75 Kitaifa wakati Shule ya Msingi Eden ni ya 4 Kiwilaya ya 10 Kimkoa na Kitaifa ni ya 77.
Shule za Msingi 10 dhaifu kwa kundi la watahiniwa zaidi ya 40 zimetajwa kuwa ni Muriti,Kaseni,Kazilankanda,Negoma,Mugu,Chamatuli,Mahande na Busagami zote za Ukerewe na Kidija na Mhalo zote za Kwimba.
Ufaulu wa Shule10 bora Kimkoa kundi la Watainiwa chini ya arobaini (40-)
Shule ya Msingi Musabe ya Jiji la Mwanza imeshika nafasi ya 1 kiwilaya ya 1 Kimkoa na Kitaifa imeshika nafasi ya 4.Peaceland ya Ukerewe imeshika nafasi ya 1 Kiwilaya ya 2 Kimkoa na ya 26 Kitaifa,Lowjoma ya Manispaa ya Ilemela imeshika nafasi ya 1 Kiwilaya,3 Kimkoa na Kitaifa nafasi ya 31,Lake Victoria E.M ya Buchosa imeshika nafasi ya 2 Kiwilaya ya 4 Kimkoa na nafasi ya 34 Kitaifa, Methodist ya Magu imeshika nafasi ya 1 Kiwilaya,5 Kimkoa, na 39 Kitaifa.
Central Buhongwa ya Jiji la Mwanza nafasi ya 2 Kiwilaya,6 Kimkoa na 62 Kitaifa,Winners ya Jiji la Mwanza imeshika nafasi ya 3 Kiwilaya,7 Kimkoa na 69 Kitaifa,Exodus ya Misungwi nafasi ya 1 Kiwilaya,8 Kimkoa na 71 Kitaifa,Kisiwani ya Jiji la Mwanza nafasi ya 4 kiwilaya,9 Kimkoa,74 Kitaifa na Mahawa Independent ya Jiji la Mwanza imeshika nafasi ya 5 Kiwilaya,10 Kimkoa na 75 Kitaifa.
Shule za Msingi 10 dhaifu Kimkoa kundi la watahiniwa chini ya 40 zimetajwa kuwa ni Bugatu ya Magu,Nyabuhere ya Misungwi,Mwabudi ya Kwimba,Isesa ya Ilemela,Ng’wang’hanga ya Kwimba,Kilongo ya Ukerewe,Ndagwasa ya Kwima na Itegamatu ya Kwimba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.