Watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Makao Makuu wamepata elimu juu ya tahadhari ya majanga ya moto iliyotolewa na Kaimu Kamanda wa jeshi la zima moto A.S.F. Aguatino Magere kwa kushirikiana na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Zimamoto Mkoa wa Mwanza.
Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo hayo kamanda Magere amesema lengo ni kuhakikisha wanatoa elimu hii ili kupunguza ajali za moto maeneo mbalimbali.
" Kazi yetu ni kuhakikiaha tunatoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto pamoja na ukaguzi na kuishauri serikali kwani tumepewa dhamana kwa niaba ya Kamishna Jenerali,alisema Kamanda Magere.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Christopher Kadio akielezea juu ya kunufaika na elimu ya kukabiliana na majanga ya moto amesema amefurahia sana mafunzo hayo kwani yamewajengea uwezo wa ufahamu wa namna ya kukabiliana na majanga hayo pindi yanapotokea kuomba mafunzo yawe endelevu.
Aidha Kadio amemwagaiza Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali watu Baraka kuweka mpango mkakati kwa ajili ya madereva ili kujiweka sawa katika kukabiliana na majanga ya moto yanayoyoweza kutokea katika vyombo vya moto wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.
Akizungumza baada ya kupata mafunzo hayo mmoja wa watumishi wa Ofisi hiyo ambaye ni afisa Manunuzi Josepha Tarimo amesema ni mazuri kwani kabla ya elimu hiyo walikuwa hawajui matumizi sahihi ya vifaa vya uokoaji.
"Kwa sasa tumepata elimu, mafunzo tuliyopata tumeelekezwa vizuri sana namna ya kujiokoa na kuwaokoa watu wengine wakati yanapotokea majanga ya moto pia naomba elimu hii iwafikie makundi mengine,alisema Tarimo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.