Mashindano ya urembo ngazi ya Mkoa yanayojulikana kwa la jina Miss Mwanza 2018 yameanza kupamba moto kwa washiriki ambao wako kambini huku wakijitokeza kushiriki kazi mbalimbali za kijamii katika maeneo tafauti tofauti .
Mashindano inatarajiwa kushika kasi July 6 mwaka huu katika eneo la Rock City Mall jijini Mwanza ambapo tayari warembo 14 wako kambini wakiendelea kujifua .
Akitoa rai kwa walimbwende hao Mkuu wa M koa wa Mwanza John Mongella aliwataka kuwa mabalozi wazuri wa kuutangaza Mkoa wa mwanza, kuwa vijana wanaojiamini na kuishi ndani ya ndoto zao ili kufikia malengo waliojiwekea na kufikia mafanikio yao.
Pia aliwataka kuwa mabalozi watakaoleta mabadiliko ndani ya jamii hivyo watumie fursa zilizopo na wawe na imani kuwa wote ni washindi, kwa niaba ya wananchi wanaowategemea kuipeperusha vyema Mwanza na kutwaa taji la Miss Tanzania na kutambua kukata tamaa ni adui mkubwa wa maendeleo.
Naye Pamela Irengo Mkurugenzi wa Kampuni ya Mepal Management ambao ni waandaaji wa mashindano hayo alisema wao wamejipanga ipasavyo kulifanikisha ilo huku akielezea kuwa halfa hiyo itapambwa na wasanii kama Nandy,Aslay huku Jokate na Hamis Mabeto kuwa miungoni mwa majaji watano kwa usiku huo.
“Kila idara imekamilika kuanzia zawadi kwa mshindi ambayo itatolewa pale pale hadharani, pia tunatambua umuhimu wa washiriki wote 14 hivyo siku hiyo tunatoa zawadi kwa washiriki wote kwa kujitoa kwao na kuacha majukumu yao ukizingatia wengine bado wanafunzi," alisema Irengo.
Anastazia Anthony ni mmoja wa washiriki wa kuwania taji la Miss Mwanza alisema kuwa lengo lake ni kushinda taji hilo na kuhamasisha jamii kuweza kutambua umuhimu wa mashindano hayo na kuachana na imani potofu ya kuyachukulia kuwa ni uhuni bali wawe chachu ya kuwaunga mkono watoto wao na kuacha tabia ya kutowaruhusu kushiriki mashindano ya urembo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.