MWANZA BILA YA WATOTO WA MITAANI INAWEZEKANA: RC MAKALLA
*Kampeni maalum ya mchukue mtoto mrejeshe kwa wazazi wake imeanza Mwanza*
*Zaidi ya watoto mia tano wamerejeshwa nyumbani*
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CPA Amos Makalla amesema Ofisi yake kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wapo katika kampeni maalum ijulikanayo kama 'Mchukue mtoto mrejeshe kwa wazazi wake' yenye lengo la kuwaondoa watoto mitaani na kurudi kwenye malezi bora.
Akizungumza leo kwa niaba yake na kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amesema kupitia kampeni hiyo kuna matarajio ya kupata matokeo chanya huku wakiwa wamefanikiwa kuwarejesha kwa wazazi wao zaidi ya watoto mia Tano.
"Mhe. Mwenyekiti wa Kamati kampeni hii tunashirikiana vizuri na wadau wa maendeleo wanaojishughulisha na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, kabla ya kuwarejesha huwa tunajiridhisha sababu za watoto hao kutoroka nyumbani kwao," Mhe. Makilagi
Makilagi amesema kwenye Stendi ya mabasi ya Nyegezi wameweka dawati maalum ya Ustawi na kufanikiwa kuwarejesha nyumbani watoto 223 na sasa wapo mbioni kuyaweka madawati mengine kituo cha mabasi Nyamhongolo, bandarini na eneo la Kamanga Feri.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mwanaidi Hamis amesema Serikali inaendelea kuiboresha miundombinu yote iliyo chini ya Wizara hiyo kikiwemo chuo cha Maendeleo ya Jamii Misungwi zilizotokewa shs bilioni 2.2 kujenga bweni la wanafunzi.
"Tayari zimetolewa shilingi Milioni 350 kuanza kujenga msingi na katika ziara hii waheshimiwa wabunge wa kamati hii watapita kukagua ujenzi huo", Amesema Naibu Waziri.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Dodoma, Mhe. Fatma Tawfiq amebainisha jukumu la jamati yake ni kupita kwenye miradi yote na kujiridhisha kuona thamani ya fedha zilizolengwa zimeendana na kilichokusudiwa.
"Sisi wabunge ndiyo tunapitisha bajezi za Serikali na kutoa ushauri pia kwenye miradi iliyokusudiwa ya kuwaletea maendeleo wananchi, hivyo ziara hii ina maana kubwa," Mwenyekiti wa kamati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.