SERIKALI IMETENGA SHS BILIONI 972 KUJENGA KAMPASI ZA VYUO VIKUU NCHI NZIMA- WAZIRI MKENDA
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga amesema Serikali imetenga jumla ya shs bilioni 972 kwa ajili ya kujenga Kampasi ya vyuo vikuu mikoani kote lengo likiwa kuwasogezea karibu wananchi huduma ya elimu ya juu na kuharakisha kasi ya maendeleo nchini.
Akizungumza mapema leo Disemba 13, 2024 kwa niaba ya Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia katika mahafali ya 18 duru ya pili kwa wahitimu wa Taasisi ya Teknolojia Dar e-s-Salaam Kampasi ya Mwanza iliyofanyika kwenye ukumbi wa Rock City Mall wilayani Ilemela, Naibu Waziri Mhe. Omari Kipanga amebainisha tayari Mwanza Kampasi ya chuo cha ardhi kipo mbioni kujengwa huko wilayani Sengerema.
Amesema mpango huo ni maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na wao kama wizara wana wajibu wa kusimamia na kuhakikisha vyuo hivyo vinakamilika kwa ubora na wakati.
"Hizi fedha zitakwenda kuboresha maeneo mengi ikiwemo mfumo wa Tehema, wahadhiri wa vyuo vya Serikali na binafsi watapata nafasi ya kusomeshwa na maeneo mengine mengi muhimu, "Naibu Waziri
Aidha ameipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar-s-Salaam DIT Kampasi ya Mwanza kwa kuendelea kuzalisha wataalamu ambao wameleta maendeleo chanya katika sekta ya viwanda na Serikali imewekeza kwenye Taasisi hiyo ili izidi kuwa mahiri katika utafiti na kuwa na wataalam bora wa ngozi.
Akitoa salamu za Mkoa wa Mwanza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa,mkuu wa Wilaya ya Ukerewe comrade Christopher Ngubiagai amebainisha kutokana na mkoa huo kuwa eneo la kimkakati uwekezaji wa Elimu ya juu ni lazima upewe kipaumbele.
"Nichukue fursa hii niwapongeze wahitimu wetu,nawasihi sana muwe mabalozi wazuri wa mageuzi ya kiuchumi hasa katika eneo la viwanda ili mliletee Taifa maendeleo",Ngubiagai.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.