Wadau wa Maendeleo wamekutana Mwanza katika kikao kazi cha kukusanya maoni,Taarifa na Takwimu katika zoezi la Tathmini ya Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000) na Mkakati wa Utekelezaji (2005) ili kuendana na wakati kwa ajili ya kutoa ufumbuzi wa changamoto za sasa.
Akiongea katika kikao kazi hicho Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Idara kuu Grace Mwangwa amesema zoezi litahusisha kukutana na wadau mbalimbali katika ngazi zote hii itasaidia kuwa na sera shirikishi inayozingatia masuala yote muhimu.
"Tumefikia kipindi tumeona kwamba tunahitaji kufanya tathmini,sera hii tumeitumia takribani kwa kipindi cha miaka 19 na ni mambo mengi yamebadirika ukiangalia sasa hivi tunaongelea maswala ya uchumi wa viwanda,uchumi wa kati,kwa hiyo tumeona ni wakati muafaka kuofanyia tathmini tupate maoni kutoka kwa wadau mbalimbali jinsi ilivyokuwa inatekelezwa, takwimu za utekelezaji na maoni ni nini kifanyike ili tuje na sera ambayo itatufikisha katika uchumi wa kati tunapoenda katika maswala ya viwanda," alisema Mwangwa.
Kwa upande wake Profesa Linah Mhando ambaye ni Mtaalam elekezi amesema ni muda sasa kuna uhitaji wa kuhuisha sera hii kwa sababu imepitwa na wakati tuliopo sasa.
"Chimbuko la sera hii ni Tamko la Beiging ambapo Nchi yetu ilijikita katika mambo matano kwa wakati ule ambayo ni kuangaliajinsi gani tunaweza kuwa na sera ambayo itaangalia changamoto wanazozipata wakina mama kwa wakati huo wa mwaka 2000 ndo maana tumeona kuwa hata jina lenyewe la sera limepitwa na wakati," alisema Profesa Mhando.
Awali akifungua kikao hicho kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Emil Kasagara amesema kikao hicho kina malengo ya kufanya tathmini ya utekelezaji wa maswala ya Usawa wa Jinsia na Uwekezaji Wanawake katika kufikia maendeleo jumuishi hususan katika Sekta ya Afya,Elimu, Kilimo na Maswala ya Kifedha.
"Kukusanya Taarifa na Takwimu zitakazowezesha kuandaa Rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Jinsia kwa kujibu mahitaji ya sasa na kutatua changamoto zilizopo,"alisema Kasagara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.