Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) imesema imeandaa utaratibu wa kuwatuza watoa huduma bora za mawasiliano nchini lengo ikiwa ni kuchochea ufanisi wa ubora wa huduma zinazotolewa na kampuni za mawasiliano.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA, Mhandisi James Kilaba wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungwa mkutano wa nchi sita za uanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zilizokutana jijini Mwanza kwa lengo la kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja juu ya gharama za kupiga simu, kuimarisha mashirika ya posta na teknolijia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).
Nchi hizo ni Kenya, Burundi, Rwanda, Tanzania , Uganda na Sudan Kusini ambapo watalaamu wa TEHAMA na wajumbe wa bodi kutoka nchi hizo wamehudhuria na kuazimia mambo 11 ambayo watayatekeleza kwa mwaka mmoja na kuwasilisha utekelezaji wake mwaka 2020 watakapokutana.
Mhandisi Kilaba alisema kutokana na sekta ya mawasiliano kuwa nyenzo muhimu kwenye harakati za maendeleo itaaanza kuwatuza watoa huduma bora za mawasiliano ukiwa ni mkakati wa kuchochea ufanisi na utoaji ubora wa huduma ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini
Alisema kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na kampuni za mawasiliano kwa kuwezesha kuunganisha watu na kurahisisha shughuli za kijamii katika maisha ya kila siku ikiwemo biashara kupitia mfumo wa kidijitali, ni muda muafaka TCRA kuonyesha shukrani zake.
Alisema tuzo hizo zitatolewa kwa watoa huduma kwenye sekta ya mawasiliano wa ndani ya nchi kabla ya kushirikisha nchi wanachama wa EAC.
“Sekta ya mawasiliano nchini kupitia ubunifu wa kidijitali umewezesha makampuni yanayoendesha biashara hiyo umeleta mapinduzi makubwa na kurahisisha maisha ya wananchi na hivyo kuchangia kukua kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.
“Tuzo hizo zitawafanya watoa huduma waone kufanya kazi pamoja na mamlaka , watajua mchango wao unathaminiwa, watanufaika na maboresho ikizingatiwa ushindani utakuwa endelevu,”alisema.
Awali, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Isaack Kamwelwe alifungua mkutano wa 23 wa Taasisi ya Mawasiliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kusema sekta ya mawasiliano kwa muda mrefu imekuwa ni nyenzo nzuri ya kila eneo la masilahi ya wananchi.
“Tuzo zitachochea ufanisi na kwa miaka 20 hatujafikiria kuwatuza watoa huduma wetu wa sekta ya mawasiliano, kutokana na kugusa wananchi wa maeneo mbalimbali mijini na vijijini.
“ Serikali imekubali utoaji wa tuzo hizo kwa watoa huduma na utasaidia kutoa unafuu kwa watumia huduma za mawasiliano katika dunia ya sasa ya uchumi wa kidjitali.
Aalisema mitandao ni muhimu na ndio uchumi wenyewe ikizingatiwa fedha nyingi zinatembea kwenye mifumo hiyo mbalimbali ikiwemo ndege, meli na maeneo mengine hivyo nchi haiwezi kufanikiwa kwenye uchumi wa kidijitali bila mitandao.
Mkutano huo wa 23 wa EACO uliofanyika wenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania (BOT),Tawi la Mwanza na kushirikisha 150 kutoka nchi sita wanachama wa EAC.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.