Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) imekanusha kuipendelea television ya Taifa(TBC) kiliko chaneli nyingine zilizo hapa nchini.
Akitoa walisilisho kuhusiana na chaneli za maudhui yanayotakiwa yatolewe bila kulipia kwa viongozi na wadau mbalimbali mkoani Mwanza , Mkuu wa Kanda ya Ziwa TCRA Mhandisi Francis Mihayo alisema, si kweli kama malalamiko ya wananchi yanayosema t?TCRA inapendelea TBC.
“Baada ya kutoa maagizo ya kuzitoa zile chaneli kwenye vizimbuzi ambavyo haviruhusiwi ndipo yakaja malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali kwamba tunapendelea TBC sio kweli,hayo ni makubaliano ya kila nchi nenda nchi za Kenya au Uganda wanayo,kwahiyo kila nchi ilikubaliana chaneli ya taifa iliyopendekezwa na taifa husika lazima ibebwe kwenye visimbuzi vyote”alisema Mihayo.
Aliongeza kuwa,Tanzania kuna makampuni sita , visimbuzi vya star media, continental digiteki na kizimbuzi cha Tingi ni makampuni yaliyopewa dhamana ya kubeba chaneli tano za bure ambazo zilikuwepo wakati wa anolojia na cheneli zitakazozidi kwenye hizo tano zitaruhusiwa kulipiwa na yakaja makampuni ambayo ukitaka kuangalia chaneli yoyote lazima ulipe ambayo ni dstv, zuku na azam.
“Kwa mujibu wa sheria ya shirika la mawasiliano duniani wakati tunakubaliana kutoka anolojia kwenda dijitali ilikubalika kwa kila nchi husika ni lazima ibebe zamana ya kurusha television ya taifa pasipo kulipisha kitu chochote ndipo mkanganyiko ulipotokea,”alisema Mihayo.
Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za jamii mkoani Mwanza, Hamidu Said alisema alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wanajiuliza kwanini wanafungia vizimbuzi na kusababisha wakose habari lakini baada ya kuhudhuria kikao cha TCRA ameelewa na kuwataka wanaopotosha waache maana wanaumiza vichwa vya watu.
Akiwakilisha waandishi wa habari mkoani mwanza, Albert Sengo alisema sheria zinazosimamia utendaji wa vyombo hivo, hazina budi kufuatwa kadri miaka inavyosonga na zikionekana haziwapi manufaa wadau hao, hawana budi kurudi tena mezani na kuzijadili kwa ajili ya kuzifanyia marekebisho kuliko wamiliki hao kufanya maamuzi yao ambayo baadaye huwagarimu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkoa wa Mwanza, 2 Regional Drive
S.L.P: 119, Mwanza.
Simu: 028-2501037
Simu ya Mkononi: 028-2501037
Barua Pepe: ras@mwanza.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Mwanza . Haki zote zimehifadhiwa.